Numbisa
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 348,970
- 1,252,247
Dawa za kupaka zenye steroidi husharabiwa mwilini na kuingia katika damu, na kiasi kinachosharabiwa hutegemea na ukubwa wa eneo la ngozi mtu anapaka na kiasi cha dawa anachopaka kwenye ngozi. Zile zenye uwezo wa chini husharabiwa katika maeneo mengine ya ngozi isipokuwa kiganja, lakini zile zenye uwezo wa juu husharabiwa kwenye ngozi na pia katika kiganja. Kiasi kikubwa cha dawa husharabiwa zaidi katika maeneo ambayo ngozi ni nyembamba, mfano karibu na macho, sehemu za siri na sehemu za mikunjo ya ngozi.