Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Dawa za kupaka zenye steroidi husharabiwa mwilini na kuingia katika damu, na kiasi kinachosharabiwa hutegemea na ukubwa wa eneo la ngozi mtu anapaka na kiasi cha dawa anachopaka kwenye ngozi. Zile zenye uwezo wa chini husharabiwa katika maeneo mengine ya ngozi isipokuwa kiganja, lakini zile zenye uwezo wa juu husharabiwa kwenye ngozi na pia katika kiganja. Kiasi kikubwa cha dawa husharabiwa zaidi katika maeneo ambayo ngozi ni nyembamba, mfano karibu na macho, sehemu za siri na sehemu za mikunjo ya ngozi.
 
Madhara katika ngozi yanayosababishwa na utumiaji holela wa steroidi za kupaka yatategemea na kiasi anachopaka mtumiaji na uwezo wa steroidi anayopaka, lakini madhara haya kwa ujumla ni kama ifuatavyo; kupungua kwa kinga ya ngozi, ambapo itapelekea mtumiaji kupata uambukizi wa fangasi hata bakteria katika ngozi kwa urahisi, na kwa uchache pia malengelenge na hata mkanda wa jeshi.
 
Husababisha matatizo kama chunusi na ukavu wa ngozi. Ngozi kuwa nyembamba ambayo hupelekea michiri, ngozi kuchubuka kwa urahisi, rashezi kuzunguka mdomo, kupoteza nywele na kuungua jua kwa urahisi. Kutanuka kwa mishipa ya damu, ambayo husababisha kuonekana kwa mishipa ya damu katika ngozi,pia wekundu katika ngozi huonekana mtumiaji anapoacha kutumia.
 
Dawa hizi zaweza kuleta madhara mwilini endapo zitatumika kiholela.Kiasi kikubwa cha dawa za kupaka zenye steroidi,mojawapo au zaidi kutoka makundi ya steroidi, husharabiwa katika kiwango ambacho huathiri kazi za tezi ya adrena. Tezi hii inahusika na utengenezaji wa steroidi za asili mwilini, ambazo ni muhimu katika kuiweka miili yetu katika afya njema . Steroidi hizi katika dawa za kupaka zinaposharabiwa na kuwepo mwilini, mrejesho wa taarifa kutoka katika ubongo hupelekwa katika tezi ya adrena, na tezi hii huacha kutengeneza steroidi za asili.
 
Endapo mtumiaji ataendelea kutumia dawa hizi kwa muda mrefu, tezi hii husinyaa kwa kuwa haifanyi kazi kwa muda mrefu. Endapo mtumiaji ataacha kwa ghafla matumizi ya steroidi hii atakuwa mgonjwa na udhaifu wa mwili utakuwa dhahiri,na endapo ataendeleza matumizi ndivyo atazidi kuathirika kadri siku zinavyosonga. Madhara atakayopata mtumiaji holela endapo kiasi kikubwa kitasharabiwa ni ugonjwa ujulikanao kama Cushing syndrome, dalili za ungonjwa ni uso wa mviringo, kuota nundu ya mafuta kati ya mabega.Alama za michirizi katika ngozi ambazo husababishwa na ngozi kuwa nyembamba na kutanuka, au kutanuka kwa mishipa ya damu
 
Pia kukusanyika kwa maji mwilini(edema), shinikizo la juu la damu, udhaifu wa mifupa na mara chache pia kisukari. Matibabu ya ugonjwa ni uangalizi wa karibu na jinsi ya kumwachisha mgonjwa matumizi ya steroidi, ili kurejesha mfumo wa asili.Matibabu huwa na mafanikio endapo mtumiaji atawahi kutibiwa.
 
Steroidi katika dawa hizi husharabiwa na kupita placenta. Kwa hiyo mama mjamzito awe makini na kupata ushauri wa daktari. Steroidi pia hutolewa katika maziwa ya mama anayenyonyesha. Uangalizi maalumu huhitajika endapo mama anayenyonyesha atakua anatumia dawa hizi. Kwa watoto, steroidi huathiri ukuaji wa mtoto, kwa hiyo watoto ni kundi ambalo pia huhitaji ungalizi maalumu katika matumizi haya ya dawa za steroidi za kupaka.
 
Kuna vipodozi vyenye steroidi ambavyo huuzwa kinyume cha sheria, steroidi hizi katika vipodozi hivi hupatikana katika makundi ya steroidi tuliyoyaona awali. Madhara yake ni sawa pia kama tulivyoyaona hapo awali.Kipodozi maarufu ambacho hutumika sana na kinamama ni Caro®light (kipodozi kilichopigwa marufuku). Chukua tahadhari endapo unaamua kubadilisha aina ya kipodozi. Wasiliana na mfamasia au mtaalamu wa ngozi endapo una mashaka na aina mpya ya kipodozi unachotaka kutumia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…