Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Endometriosis hutokea pale seli na tishu zinapojijenga nje ya tumbo la uzazi na seli hizo na tishu zinakuwa na tabia ya kawaida ya
kujijenga na kuongezeka unene, na kubomoka wakati wa mzunguko wa hedhi kama zile zilizojijenga ndani ya mfuko wa uzazi. Lakini tofauti ni kwamba seli hizi na tishu zilizobomoka na zilizo nje ya tumbo la uzazi, hazitaweza kutoka nje kama damu ya hedhi anayopata mwanamke mwanzo wa mzunguko mpya.
 
Endapo tatizo hili litaathiri ovari, zaweza kusababisha uvimbe ( kwa kitaalamu unajulikana kama endometriomas). Tishu jirani na uvimbe nazo zaweza kuathirika na kupata kovu au tishu kushikamana isivyo kawaida. Hii huweza kupelekea hata kuziba kwa mirija ya kupitisha mayai ya uzazi.
 
Hakuna sababu zilizo thabiti kuonyesha ni nini hasa kinachosabisha ugonjwa huu, lakini zifuatazo ni sababu zinazoweza kusabisha ugonjwa huu:-

Sababu za kigenetiki-Ugonjwa huu huweza kuwa katika familia fulani, na vinasaba vya ugonjwa vyaweza kurithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine.
 
Matatizo katika mtiririko wa hedhi- Mtiririko wa kinyumenyume wa hedhi (retrograde menstrual flow) ndio sababu kubwa ya mwanamke kupata ugonjwa huu, hii ina maana kwamba mtiririko wa hedhi wa tishu za ukuta wa kizazi uliobomoka hurudi na kuingia katika mirija ya mayai na husababisha tatizo kusambaa katika viungo vingine kama nyonga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…