Ndege hula vijidudu na ndicho chakula chake kikuu, anapokufa vijidudu humla ndege... na hayo ndio maisha, usimdharau kiumbe kwa udhaifu wake, kesho atakushinda kwa nguvu, uaibike.
Watu wanamsifu mbweha wakati ni hatari kwao, na wanamdharau mbwa wakati ni mlinzi wao. Ajabu dunia hii! Watu wengi wanawadharau watumishi wao, wakati wanawatumikia; na wanawatukuza wengine wakati wanawadunisha.
Bwana mmoja alimwambia swahiba wake huku akishangalia makasri ya watu: Sisi tulikuweko wapi wakati hawa wanapewa utajiri huu!!!? Swahiba wake akampeleka hospitalini kwa wagonjwa na kusema: Sisi tulikuweko wapi wakati hawa wanapewa maradhi haya!!!? Mshukuru Mwenyezi Mungu kwa hali yoyote anayokujaalia, na kwa riziki anayokuruzuku na uzima aliokutunuku.
Samaki anayefumba mdomo wake, hashikwi na ndoana ya mvuvi, jitahidi kufumba mdomo wako kwani kuna watu wengi wana hamu ya kukutia ndoana kwa makosa yako