Ingawa tunaishi katika hali ya kujilinganisha au kujifananisha , Hii hali itahitaji mafunzo makini ya ubongo, lakini kusema kweli unahitaji kuacha tabia hii mbaya ya kujifananisha na mwingine
Acha kuingiza sumu hii mbaya kwenye ubongo wako na kwenye roho yako unapojilinganisha na wengine. Hiki kitu kinatokea wakati tunapohitaji mafanikio katika umri wetu, katika ndoa zetu, kumiliki mali na kuwa na watoto kwa kutamani na kutaka kuwa kama wengine
Kusema kweli ni kwamba kujilinganisha unapoteza uwezo wako mwenyewe, unaweka uwezo wako katika mikono ya mwingine. kutaka kitu kama walichonacho watu wengine. Kusikiliza kuhusu watu wanasema nini juu ya maisha yako. kutoridhika na ulicho nacho.
Tambua kuwa kila mtu ana safari yake tofauti. hatulingani. Kuna mtu anaweza kufanikiwa akiwa na miaka 21. Wengi wanaweza kufanikiwa wakiwa na miaka 41. Kila mtu hupata mwenza amtakaye kwa wakati tofauti. na kupata watoto kwa wakati tofauti. Kujilazimisha kuamini kuwa ni lazima kuolewa chini ya miaka 30
ni kitu cha kijinga na kitakupa mawazo na hata kuchanganyikiwa. kama mtu amefanikiwa katika umri huo ni yeye sio wewe. Au kutaka kuoa mapema hata bila ya kupata kazi , nyumba, hio sio akili hata kidogo. Fuata moyo wako. kama ukiwa tayari fanya . kama bado usiige mtu. subiri wakati wako utafika.
Maisha ni zaidi ya kuoa au kuolewa. na ni zaidi ya mafanikio unayojilinganisha nayo. Maisha ni kuhusu kuwa mtu bora.. Ni kumkubali kila mtu ambaye anakuja na kuondoka katika maisha yako. Ni kuishi maisha ya ukamilifu.
Ni kufanya makosa na kujifunza kutokana na makosa hayo. Ni kuhusu kumpenda mtu ambaye sio sahihi, wakati mtu ambaye ni sahihi atakuja wakati ambapo umejifunza kuwakubali watu. Ni kuhusu kujiweka tayari katika changamoto utakazokabiliana nazo.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.