Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kwa hio Acha kabisa kusikiliza kila kitu, acha kujilinganisha na mtu mwingine yeyote. Tambua kuwa wewe ni wa tofauti, kila mtu ana wakati tofauti. Safari yako ni tofauti.

Maisha hayajaisha mpaka yatakapoisha, Maana yake kila mtu anaweza kurejesha uwezo wake uliopo ndani yake.
 
Hakuna mwisho, kama utaona mwisho tambua kuwa kuna kona, songa mbele usirudi nyuma, Hio ni kona tu, Utapita na utaona njia sahihi uliotarajia kwa kiasi.

Kama wewe umekuwa mtu wa kujilinganisha kwa kila kitu, na kila mtu. unajaribu hili unashindwa , unajilinganisha na mwingine pia. Unasikiliza watu wanasema nini , wanawaza nini juu yako.Huridhiki na ulichonacho, Tambua kuwa upo kwenye hivyo vizuizi.
 
Anza kurudi katika ufahamu wako. Kumbatia uhalisia wa msamaha wa Mungu, Usijihukumu, Jifunze kutokana na makosa yako, Rejesha muda uliopoteza kwa kujilinganisha. Anza Kujisamehe mwenyewe, komboa wakati, Badilisha mtazamo wako, kuwaza kwako, kutenda kwako. Weka akili yako vizuri. Tumia muda wako vizuri.
 
Fanya kitu unachokipenda, shauku ya moyo wako. Kitu ambacho utafanya bila ya kutumia jasho. Jitambue. Muhusishe Mungu, Pata mtu ambaye utajifunza kwake. Hata kama ni ndoa, tafuta ni ndoa ipi ya kujifunza, Tafuta taarifa. Gundua vitu vipya.

Acha kuingiza sumu mbaya ya kujilinganisha na mtu, huyo sio wewe. Kumbuka kuwa wewe ni wa tofauti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…