Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Jaribu kuwa vizuri sehemu ambayo sio nzuri.

Mara nyingi maisha huwa yanachanganya, wakati mwingine tunakosa pesa. hatuwezi hata kununua kitu ambacho tunakitaka. Kama una kitu unataka kifanikiwe utahitaji uweze kuishi katika hali ambayo sio nzuri ili ufanikishe.
 
Maisha ni uhakika. Endelea.

Mambo hutokea. Nilifikiri nimefanikiwa, nilipokuwa na kazi nzuri, nyumba nzuri. Lakini siku moja ikatokea moto, vitu vyote viliungua. Na wakati huo nimejikuta nina miaka 40, halafu nilijikuta ni mjamzito, nilichanganyikiwa. lakini niliamua kuhama mji. Nilichukua yanayowezekana tu kichwani mwangu. Kila kitu kibaya kinachotokea hufungua mlango wa kitu kizuri.
 
Hii ni kweli , kwa sababu huwezi kurudi nyuma, bali ni kuanzia hapo ulipo. Kama hutafanya maamuzi yako sasa hivi hapo ulipo, hutakuwa na kitu cha kuonyesha. Lakini utabaki kupost facebook, na kukaa kwenye TV shows
 
Jitolee Kwa Mtu .

Kama kuna kazi unayoipenda, jitolee kufanya bure.Kwa sababu mahali hapo utaanza kupata uzoefu. Ndoto yako haitaweza kutimia kama hutaweza kwenda kufanya kazi ya aibu kwanza. Kazi ya kuchafua mikono yako. Unaweza usielewe, lakini ndio kazi zinazofungua milango mikubwa.
 
Fungua Mlango.

Nafasi huenda inabisha hodi lakini kama hutafungua mlango, utawezaje kuifurahia hio kazi? Chukua nafsi kabla ya kuanza kupata malipo. wakati mwingine inaweza kuwa sio wakati sahihi. Lakini haina shida. wewe fungua mlango wa nafasi yako kwa kutumia mlango wa mtu mwingine ulio wazi tayari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…