Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

9.Hauhitaji kuwa na muda au mtindo wa maisha kama walionao watu wanaokuzunguka.

Huhitaji kufanana na mtu, huhitaji kukaa nje masaa yote bila sababu, huhitaji kuwa na wasichana wengi au wavulana wengi kwa wakati mmoja, huhitaji kujiona huna Elimu kama fulani, Huhitaji kujiona masikini, huhitaji kujishusha kwa hali yoyote ile. Chuo kizuri ni kujitambua mwenyewe na kujiboresha kwa mtindo wako wa peke yako. rahisi na haina vikwazo.
 
12.Usifikiri kila ugomvi ni mwisho wa mahusiano.

Baadhi ya mahusiano wanashindwa kukabiliana na hili, lakini yaliyo ya kweli yanaweza. Wape watu faida ya kutambua kuwa mashaka yao yatawafanya waelewe mahali ulipotokea.
 
14.Jaribu kitu ambacho hujawahi kukifanya kabla na uone utajisikiaje.

Vaa vizuri, tembea kwa ujasiri, kama ni msichana vaa viatu virefu kidogo, na kisha pita mbele za watu . jisikie vizuri. utajipenda jinsi ulivyo, fanya hivyo mara moja utatambua kwamba unazidiwa na hisia nzuri. Soma kitu kipya, gundua jambo jipya kila mara.
 
16.Usiogope Kuacha kazi ili kufanya kitu kingine unachokipenda.

Kwa sababu kazi yako imekuwa kama kitu kinachokunyonya damu, ni vizuri kuondoka katika kazi hio. Lakini angalizo.Usiache kazi kama huna kazi nyingine, kama huna maono , kama huna ndoto. Lakini pia usiingie kwenye mtego wa maisha.
 
17.Jaribu na uache kujihisi huna bahati kwa kukua ukiwa na wazazi wako.

Ni kawaida kutaka kuoa au kuolewa, na kusherehekea, na kupata watoto. Ongea nao kuhusu hilo usione aibu. maana wao wanakutazama kwa jicho la tofauti sio unavyofikiria wewe.
 
19.Ni sawa Kumpenda Rais Magufuli, Ni sawa kumchukia pia . ni sawa kumsaidia na kumuombea.

Hivi ndivyo ilivyo katika kupenda na kutopenda. Unaweza kupenda ladha tofauti ya ice cream. kwa sababu hakuna watu wawili ambao wanaweza kuwa na mawazo sawa. Usimlaani mtu kwa sababu ya kutokubaliana na Siasa yake , utajitakia matatizo bure. Ishi kwa usalama .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…