Utakuwa Umewahi kusikia au unasikia watu wakijilaumu kuwa hakufanya kitu hiki akiwa na nguvu zake. Mfano ;Hakujua nini cha kufanya mapema kabla ya kufikia umri alio nao sasa.
Nilikuwa nimejilaumu mapema kwa kutokufuata hamu yangu .Angalau sasa najiuliza maswali ninayohitaji, nilikuwa nani, nilitakiwa kuwa wapi, na kufanya nini.
Unawezaje kujithibitisha? au Uthibitisho wako ni upi?
Katika mtindo ulio rahisi sana, Ni katika kufanya mambo mazuri au kuwa na tabia nzuri kwa ajili yako mwenyewe. Itakuthaminisha kwa jinsi unavyoamini kuwa unalo kusudi katika maisha yako. Ni katika kuwa na Ujasiri ndani yako.
Uwe mwenye shukurani. Maswali rahisi yanaweza kukusaidia kukuongoza kwenye njia sahihi na kusaidia kuthibitisha kwamba unafanyia kazi kulingana na ulichokuwa unakitaka. Ina maana kwamba kupunguza lawama ambazo unajiona hukufanya kitu miaka kadhaa nyuma.
Sasa sihitaji ujiulize maswali haya yote kila siku. Ingawa kuwa na muda mdogo wa kujitambua jinsi unavyojisikia kwa kuchagua baadhi ya maswali , yanaweza kukusaidia na kuuweka ubongo wako kwenye mafunzo ya kufikiria mambo mazuri.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.