Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Lakini katika uchunguzi mwingine wajapana hawana matatizo mengi ya kisukari na magonjwa kama ya moyo kutokana na kuwa na mafuta mwilini ya kuzidi. Ni sababu ambayo tunatakiwa kujifunza kitu au vitu kutokana na mtindo wao wa maisha katika afya yao ya mwili na akili.
 
Kwa Nini Kunywa Maji Ni Muhimu Sana?

Asilimia kubwa mwilini mwako imetengenezwa na maji, kwa hio ni muhimu kutunza kwa kutumia maji ya kutosha ili mwili ufanye kazi kwa usahihi. Wakati kiasi cha maji yanayohitajika yasipotosha. utakutana na magonjwa ya muda mfupi au ya muda mrefu.
 
Nitayafanyaje Maji Yawe Ni tiba ?

Hii imehakikishwa kuwa ni njia nzuri ya kutibu matatizo ya mwili , kama mzunguko wa hedhi kwa kina mama, macho kuona vizuri. pia utajisikia vizuri siku nzima kwa kufuata mtindo huu wa kunywa maji kama tiba
 
1.Kuondoa Sumu Mwilini

Kwa kadri unavyotumia maji, unarahisisha mzunguko ndani uwe vizuri. usiku mwili hutengeneza sumu, kwa hio unapokunywa maji asubuhi wakati tumbo liko wazi , utaflush madhara yote ya sumu, na kuacha mwili wako uwe fresh na wenye afya.
 
2.Inaboresha Metabolism

Kutumia maji wakati tumbo likiwa wazi huongeza kiasi cha metabolism . ni muhimu kwa watu wale wanaofanya diet. kuongezeka kwa metabolism in maana kuongezezeka kwa digestive system. kunywa maji mara tu unapoamka asbuhi. ili kusafisha utumbo mkubwa na kurahisisha kunyonya virutubisho.
 
3.Kulazimisha Kupungua Uzito.

Unapotumia maji ya kutosha asubuhi , utaondoa sumu zote na kuboresha digestive system yako. hautasikia njaa sana, itakusaidia kupunguza uzito kwa sababu hutakula sana.
 
4.Inasaidia Kuondoa Kiungulia

Unahangaika na kiungulia kwa sababu ya wingi wa Acid tumboni. unapotumia maji wakati tumbo lipo wazi , acid hizi husukumwa chini na tatizo huondoka. pia hiki ni kianzio cha kuamsha kichwa chako kwa ajili ya chai.
 
5.Hupunguza Mikunjo Mwilini

Mikunjo mingi husababishwa na kukosa maji ya kutosha. lakini kama utaweza kutumia maji ya kutosha hasa asubuhi , inaongeza msukumo wa damu kupita kila sehemu ya mwili ili kukuza ngozi yako na kuing’arisha.
 
6.Inasaidia Kukuza Nywele Na Kuleta Ulaini Wa Ngozi Yako.

Maji yanasaidia sana katika kukuza nywele, ndani na nje. kwa kuwa nywele pia zinahitaji maji ya kutosha ili ziweze kuwa na afya.kinyume chake ni kudumaa kwa nywele. tumia maji ya kutosha kila siku, lakini tumia maji hayo wakati tumbo likiwa wazi asubuhi.
 
7.Kuzuia Mawe Kwenye Figo Na Madhara Ya Kibofu Cha Mkojo.

Kunywa maji mara tu unapoamka ni muhimu kwa ajili ya kuzuia mawe yanayokaa kwenye figo na madhara ya kibofu cha mkojo. ni kweli kwamba kunywa maji wakati tumbo likiwa wazi yanadilute Acid zinazobadilika mawe kwenye figo. ukitumia maji ya kutosha kulingana na kiasi maalum. utajilinda zaidi kutokana na madhara hayo.
 
Back
Top Bottom