Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Tumia kidogo kuliko unachopata

Ni rahisi kutumia kuliko kutafuta; hivyo si jambo la kustaajabisha ukajikuta unapata elfu tano kwa siku lakini unatumia elfu saba. Maana yake hapa unatengeneza deni mahali la shilingi elfu mbili kila siku. Inawezekana unakula akiba au faida katika kile unachokifanya. Jifunze kutumia kidogo kuliko kile unachokipata ili uweze kutunza pesa kwa ajili ya wakati wa uhitaji.
 
Tumia vitu (huduma) vyema

Kuna huduma kadha wa kadha tunazozihitaji kila siku katika maisha yetu kama vile maji, umeme, gesi, simu n.k. Mara nyingi watu hushindwa kutumia huduma au vitu hivi vyema na kujikuta wakijiongezea gharama za maisha zisizokuwa na sababu ya msingi. Mambo unayoweza kuzingatia katika swala hili:
 
Tafuta punguzo

Mara nyingi vitu huuzwa kwa punguzo, hivyo ni vyema ukanunua vitu kwa punguzo kuliko kununua kitu katika bei halisi ili kupuguza gharama. Naamini unafahamu kuwa yapo maduka yanayouza aina fulani ya shati kwa shilingi laki tatu,
 
lakini shati hilo hilo linauzwa kwa shilingi elfu kumi na tano duka jingine. Sasa kwanini usinunue kwenye hili duka la pili linalouza shati kwa shilingi elfu kumi na tano? Epuka sifa na ufahari usiokuwa na sababu, tafuta na nunua vitu kwa punguzo ili kuokoa pesa ambazo zingepotea bila sababu.
 
Kuna hatua kadhaa unazoweza kuzitumia kujilinda na maradhi yasiyokuwa na sababu kama vile kula chakula bora pamoja na kuzingatia kanuni za afya kama vile usafi. Chukua hatua mapema ili usipoteze pesa zako hosipitalini kila siku kutibu maradhi ya tumbo au malaria ambayo ungeweza kuyazuia.
 
Acha tabia badhirifu

Kuna tabia kadha wa kadha ambazo watu wengi hawazijui kama ni moja kati ya tabia badhirifu. Tabia kama vile Kuvuta sigara, pombe, unywaji wa soda, ulaji wa pipi, kulipia michezo ya kompyuta, kukodisha filamu, kamari n.k ni baadhi tu ya tabia badhirifu. Unaweza kuepuka tabia hizi na kuokoa kiasi kikubwa cha pesa ambacho kinapotea bila sababu.
 
Rekodi matumizi yako

Kwenye suala la kutunza kumbukumbu binafsi hasa za kipesa ni suala gumu kwa watu wengi. Lakini ni vyema ukajifuna kutunza kumbukumbu za matumizi yako ili hatimaye uweze kufahamu jinsi ulivyotumia kipato chako. Kwa kufanya hivi utaweza kubaini ni wapi ambapo hukutumia pesa zako vyema na utaweza kujirekebisha wakati mwingine.
 
Fahamu kuwa kuna wakati chanzo chako cha kipato cha sasa kinaweza kukauka; hivyo kuwa na akiba kutakuwezesha kukidhi mahitaji yako kwa wakati ambao huna kipato cha uhakika au cha kutosha. Unaweza kufanya mambo yafuatayo:
 
Back
Top Bottom