Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kuna jambo limenifurahisha Sana Jana nilipokuwa Maktaba ya Mkoa wa Morogoro nilipoenda kupata Chakula ya ubongo kama ilivyo Ada yangu nika jikuta nacheka Sana Leo [emoji23][emoji23][emoji23]...... Nikaona Leo Niandike kile kilichonikuta Jana.

Jana niliingia library ya Mkoa wa Morogoro iliyopo Morogoro mjini, Nilipofika ndani ya library palikuwa kimya sana. Wakati natafuta mahali pa kukaa, nikakutanisha macho na mtoto mmoja hivi shombe-shombe mkali balaa. Akatabasamu kisha akainamia kitabu chake, akaendelea kusoma.

Moyoni nikajisemea : " FURSA "
Nikamsogelea, kwa sauti ya chini sana iliyotutosha sisi wawili tu nikamchombeza : " Habari mrembo! Ninaweza kukaa hiki kiti cha jirani yako? "

Akanijibu kwa sauti kubwa mno hakuna ambaye hakuisikia mle ndani : " SIWEZI KULALA NA WEWE, LABDA UNIROGE "

Kila mtu alinigeukia mimi na kunishangaa. Kwa unyonge nikaenda kukaa kwenye nafasi nyingine iliyokuwa wazi. Baada ya dakika mbili yule mrembo akanifuata hadi nilipokuwa nimekaa. Akiniambia kwa sauti hafifu mno : " Ninasoma Psychology, hivyo ninajua unachofikiria. Unajihisi nimekuaibisha sana..sio? "

Nikaropoka kwa sauti kubwa : " LAKI 2 KWA USIKU MMOJA TU! AH...WAPI! LABDA UNIROGE ". Kila mtu alicheka kwa sauti mle library.

Halafu nikamwambia kwa sauti ya chini mno : " ninasoma sheria, ninajua kumfanya mtu ajione mwenye hatia "

Hakujua kuwa Mimi ndie donlucchese mjoli wa jurisprudence [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom