Numbisa
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 348,970
- 1,252,247
Cha tano ni kuepuka jua kali. Unaweza ukawa unajipendezesha vizuri lakini ukiwa unapigwa na jua kali basi jua linaharibu ngozi yako na kupoteza thamani ya vipodozi vyote. Jua kali huharibu ngozi zetu na kwenda kinyume na malengo yetu ya kupendezesha ngozi. Unaweza ukaepuka jua kali kwa kushinda na kufanyia kazi zako kivulini, kuvaa nguo zinazofunika mwili wako vizuri au kupaka vipodozi vinavyoukinga mwili wako dhidi ya jua (Sun screens / Sun blockers).