EPUKA JUA KALI
Jua kali ndo hutuongezea weusi katika ngozi zetu, hutuunguza na kuongeza kasi ya kuzeeka. Hii ndio sababu watu wengi ambao shughuli zao ni kilimo na shughuli zingine za kukaa juani huwa weusi zaidi na kuwahi kuzeeka. Wazungu wanatuuzia SUN SCREEN kwa ajili ya kujikinga dhidi ya jua, bei yake sio chini ya Tsh 7,000/=. Hauwezi kujikinga dhidi ya jua kali kwa njia za asili?
Jua kali hupunguza ufanisi wa vipodozi. Ndio maana watu wengi hutumia vipodozi vya gharama kubwa na bado hawapati matokeo mazuri na kwa haraka.
Vaa nguo zinazofunika mwili wako vizuri, vaa kofia, vaa miwani. Epuka kushinda juani kwa muda mrefu unaharibu ngozi yako.