Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Unafanywa utafiti na uchambuzi yakinifu ili kujua kiasi gani cha dawa hiyo ndicho kinafaa kwa kutibu ugonjwa au tatizo husika, na kiasi gani cha dawa kinakuwa kikubwa na kinadhuru mwili wa binadamu
 
Screenshot_2017-11-08-22-56-09.png
 
Hapa ndipo tunapata aina mbili za dozi, Dozi ya kutibia na Dozi sumu. Dozi ya kutibia ni kiasi kidogo kabisa cha dawa ambacho kinatosha kwa matibabu ya ugonjwa husika, na Dozi sumu ni kiasi cha dawa ambacho ni hatari (sumu) kikitumika.
 
Hii hutegemea na uwezo wa dawa husika kukaa mwilini na kufanya kazi. Kuna ambazo huweza kukaa mwilini na kufanya kazi kwa muda mrefu hivyo hazihitajiki kutumika mara kwa mara,
 
Bila kutumia dawa vizuri huwezi kupona vizuri.

Ukitumia kiasi pungufu cha dawa (Kutumia chini ya dozi, kutomaliza dozi zote nk) vijidudu vinavyosababisha magonjwa huwa havifi vyote na hivyo kuweza kusababisha ugonjwa tena baadae. Matokeo yake ni kujirudiarudia kwa ugonjwa na hata ugonjwa kuwa sugu.
 
Ukitumia kiasi kikubwa cha dawa unaweza kuzidiwa nguvu na dawa, kuharibu viungo vyako vya mwili (kama vile ini na figo) na hata kufariki.

Hakikisha unatumia dawa zote vizuri kabisa kama ulivyoelekezwa na daktari na mfamasia. Ukipata tatizo toa taarifa kwa watu hao haraka iwezekanavyo, na si kuacha kutumia dawa bila taarifa.

Tuzisaidie dawa zetu ili zitusaidie.
 
Back
Top Bottom