Kama nilivyoeleza hapo awali kuwa ugomvi unaathiri utendaji kazi wa binadamu, je si zaidi sana masomo ya mtoto ambaye ubongo wake haujakomaa kikamilifu kukabiliana na changamoto mbalimbali za kimaisha?
Mtoto huyo awapo shuleni, walimu watakapokuwa wakifundisha wakati mwingine atakuwa hazingatii wala kuwaelewa vizuri bali atakuwa anawaza jinsi wazazi au walezi walivyokuwa wakigombana.
Nakumbuka wakati nikiwa shule ya msingi, katika somo la Kiswahili, tulisoma hadithi iliyokuwa ina kichwa cha habari “Sikulamba Sukari”. Katika hadithi hiyo kuna kisa cha mama na watoto wake.
Akawaita akawauliza, nani amelamba sukari? Kila mtoto akakataa. Kesi ikaishia hapo. Sasa miongoni mwa wale waliokuwa kwenye kesi ya kulamba sukari, akiwa darasani, mwalimu anafundisha, yeye aliwaza tukio la kulamba sukari.
Kama kawaida, kwa sisi walimu tunajua kipimo cha kutaka kujua kuwa umeeleweka au la darasani wakati unafundisha ni pamoja na kuuliza maswali kabla hujatoka darasani. Mwalimu aliuliza swali darasani linaloendana na mada yake ya siku hiyo. Akamuuliza yule mwanafunzi aliyekuwa akiwaza suala la kulamba sukari, akasimama na akajibu “sikulamba sukari
Wanafunzi wote wakaangua kicheko. Kwanini wanafunzi wenzake walicheka sana? Ni kwa sababu jibu alilolitoa halikuendana hata kidogo na swali alilouliza mwalimu. Kwanini mwanafunzi alijibu hajalamba sukari? Ni kwa sababu alikuwa akiwaza kesi ya sukari iliyotokea nyumbani.
Lengo la kutolea mfano wa hadithi hii katika makala hii ni kuonyesha jinsi ambavyo matukio ya nyumbani yalivyo na athari katika masomo ya watoto.
Ugomvi wa wazazi pia unasababisha mtoto kushindwa kujisomea awapo nyumbani. Baadhi ya wazazi na walezi wanapogombana hutoa sauti kubwa ambayo hata watoto waliolala huamka.
Kutokana na ugomvi huo husababisha hata mtoto aliye chumbani kwake hushindwa kuendelea kujisomea kama alikuwa anajisomea hasa pale anaposikia baba na mama wanagombana. Mtoto huacha kujisomea na kutega sikio nini kinaendelea kati ya wazazi au walezi wake.
Wakati mwingine mtoto hujisomea sebuleni anasikia wakigombana sehemu anayosomea mtoto. Katika hali hii mtoto hawezi kuendelea kujisomea huku akishuhudia wazazi wanagombana na hata akijitutumua kusoma hapo hapo kwenye uwanja wa mapambano ya wazazi hawezi kuelewa na kuingiza kitu katika ubongo wake.
Wakati mwingine ugomvi huo husababisha walezi au wazazi hukosa ufuatiliaji wa maendeleo ya masomo ya watoto wao. Ili mtoto afaulu anahitaji msaada wa wazazi au walezi kumfuatilia shuleni. Ugomvi wa mara wa mara kukosa ari ya ufuatiliaji na nguvu nyingi huelekezwa katika kutafuta suluhisho la matatizo yao ya ndoa.
Kama ni mama anayepigwa sana na mumewe atawaza jinsi ya kuokoa ndoa yake na kusahau wajibu wake kama mzazi wa kufuatilia taaluma ya watoto wake.
Mtoto anayekosa ufuatiliaji wa wazazi au walezi katika masomo yupo katika hatari ya kufeli kwa sababu anajiongoza mwenyewe na ni hatari kwa mtoto kujiongoza katika masuala mbalimbali ya kimasha likiwemo la elimu.
Ni kweli kuwa hakuna binadamu aliyekamilika. Kila mtu ana udhaifu wake. Kama wazazi au walezi tuchunge sana tofauti zetu ndani ya nyumba zisiwe sababu ya watoto kushindwa kitaluma. Watoto wanahitaji msaada wetu katika masomo yao, tuwape ushirikiano wa kutosha.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.