NJIA RAHISI ZAIDI YA KUPATA MATIBABU MAZURI KWA URAHISI
Hakuna kitu kibaya kama kuumwa wakati hauna pesa za kutosha na hatimaye kukosa matibabu mazuri na kwa wakati kwa sababu tu hauna uwezo. Utaumwa mara mbili – ugonjwa na ukosefu wa hela.
Kukosa pesa za kutosha kwa ajili ya matibabu mazuri na kwa wakati ni miongoni mwa changamoto ambazo zinawakabili watu wengi sana hususan ambao hawana bima ya afya na usafiri wa uhakika.
Kuweka akiba kwa ajili ya matibabu
Hii ni njia nzuri sana. Hakikisha katika kipato chako unaweka angalau akiba ya matibabu kulingana na gharama za matibabu katika eneo lako, kwa ajili yako mwenyewe na kwa ajili ya watu wanaokutegemea.
Kama umeajiriwa sekta rasmi au unaweza kujiunga na bima basi ni vyema ukafanya hivyo. Ni bora sana kuwa na bima kwani inakuhakikishia kupata matibabu bora na kwa wakati hata kama hauna pesa.
Kwa sasa kuna bima nyingi sana za afya zenye vigezo na gharama tofauti. Chagua mfuko mmoja mzuri zaidi kwako na unaoweza kuumudu kisha jiunge. Ni muhimu sana kuwa na bima ya afya.
Kwa sasa kuna bima nyingi sana za afya zenye vigezo na gharama tofauti. Chagua mfuko mmoja mzuri zaidi kwako na unaoweza kuumudu kisha jiunge. Ni muhimu sana kuwa na bima ya afya.
CHF (Community Health Fund) na TIKA (Tiba kwa Kadi) ni miongoni mwa mifuko unayoweza kujiunga nayo na kupata matibabu hata kipindi ambacho hautakuwa na pesa
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.