Alikuja mtu akiamini mimi ni mganga na kweli nikamlia fedha yake na nikamuita aje kunuia mwenyewe makaburini, akisema kama maiti huwa inarudi na yeye ugonjwa umrudie, kama hairudi na yeye apone, alipona kweli, lakini ni kwa imani kwa sababu sijui dawa yoyote ya kienyeji,” anasema Mwaimbo.
Kibinja anasema hata wenye kazi hiyo wanamjua, “Waganga wananiogopa, wananilinda, wananitetea kwa sababu huamini nafahamu vitu vingi kutokana na kuwaona wakifanya mambo yao, mchana na usiku.”