Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hutuonyesha nywele, au huambiana wenyewe kwa wenyewe duh... nywele zinachelewa kuoza na wakati mwingine hutoa mifupa na kuiweka pembeni. Wakimaliza kuchimba kaburi jipya, huichimbia pembeni na kuifukia upya.
 
Mara nyingi wanakuwa kule mwisho wa makaburi wakijichoma sindano na kusinzia kutwa nzima,” anasema Monica.

Anasema kulikuwa na mchimba kaburi aliyeitwa Kimwaki ambaye kila alipochimba na kukuta mifupa ya binadamu alituita kutuonyesha.

“Tulikuwa tunamkimbia. Mnaweza kwenda hadi mtaa wa pili kukaa kwa woga,” alisema.
 
Akishatutisha ndiyo anaitenganisha na kuiweka pembeni kabla ya kuchimba shimo dogo pembeni ya hilo kaburi la awali na kuizika. Tulikuwa tunaogopa hadi tukazoea. Akianza kuchimba kaburi juu ya la zamani kila mtu anaingia ndani.”

Makaburi kuwa gesti

Mkazi aliyejitambulisha kwa jina la Nasra, ambaye madirisha ya nyumba yake yanapakana na makaburi ya Kinondoni, anasema eneo hilo limegeuzwa kuwa nyumba ya wageni, maarufu kama Guest Bubu.
 
Huwa natamani nimwage upupu eneo lote hilo kwa sababu imekuwa kero. Watu hufika hapo jioni hadi asubuhi,” alisema.

Anasema angekuwa amepanga angehama kutokana na yanayoendelea eneo hilo.

“Unaona dirisha la chumbani nililiziba na nikatoboa huku mbele. Napata joto kwa sababu huku kumezibwa, lakini afadhali natulia kidogo,” alisema.
 
Anasema kwa hali ilivyo sasa katika makaburi hayo, kuna siku mafuvu yataelea na hasa kipindi cha mvua kwa sababu makaburi hufukuliwa, kuchimbwa na mabaki kuzikwa upya. “Wanafukua makaburi ili wachimbe mengine, kuna siku waliisahau mifupa bila kuifukia ikiwa na sanda yake tukaifukia,” anasema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…