Naye Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nasari ameandika ujumbe wake akisema wanajua sababu za Masha kuondoka CHADEMA na sio zile ambazo amezitaja, na hata hivyo wanaheshimu mamuzi yake. “Tunaojua sababu za Masha kutoka CHADEMA zile kwenye barua yake tunajua ni danganya toto, tunajua sababu na tunaziheshimu. Kuthibitisha kuwa CHADEMA imejipanga kuingia ikulu, angalia takwimu za ushindi wa madiwani na wabunge nchini kuanzia 1995 hadi sasa. Ikulu ni suala la muda, tena si mrefu”, ameandika Joshua Nasari.