Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

hughuli ya kujenga upya nchi yetu na kuhakikisha maridhiano ya taifa inaweza tu kutokea iwapo kutakuwa na uchaguzi huru na wa haki, ambao utafanyika kwa kipindi kifaacho na kitakachoafikiwa wakati wa kuunda serikali ya mpito.
 
Kiongozi wa upinzani Zimbabwe Morgan Tsvangirai amesema Rais Robert Mugabe anafaa kujiuzulu mara moja na kupisha serikali ya mpito ambayo itafanikisha kuandaliwa kwa uchaguzi huru na wa kidemokrasia.
 
Rais wa Guinea ambaye kwa sasa ndiye mkuu wa Umoja wa Afrika (AU) amekariri msimamo wa muungano huo na kusema hautakubali "mapinduzi ya kijeshi" Zimbabwe, shirika la habari la AFP limemnukuu akisema.
 
Tunataka katiba iheshimiwe na mfumo wa utawala wa kikatiba urejeshwe. Hatutakubali mapinduzi ya kijeshi.
Tunafahamu kwmaba kuna matatizo ya ndani. Haya yanafaa kutatuliwa kisiasa ndani ya chama cha Zanu-PF na si kwa uingiliaji wa jeshi."
 
Anaonekana kuchukua msimamo mkali kuliko Tume ya AU ambayo kupitia taarifa usiku wa kuamkia leo ilisema mzozo huo unafaa kutatuliwa "kwa njia ambayo itaendeleza demokrasia na kuheshimiwa kwa haki za kbinadamu".

Lakini tume hiyo haikutaja kilichotokea huko kuwa mapinduzi ya kijeshi.

Majenerali ambao wametwaa madaraka wanasisitiza kwamba hawajafanya mapinduzi ya kijeshi bali wanataka kuwakabili "wahalifu" ambao wanamzingira Rais Robert Mugabe.
 
890a8c3add2cf34d610cbe95c8c577bc.jpg
 
Kiongozi wa vijana Zanu-PF aomba jeshi msamaha
Kiongozi wa muungano wa vijana wa chama tawala Zanu-PF Kudzai Chipanga, ambaye amekuwa muungani mkono wa Rais Robert Mugabe na mkewe Grace ameomba radhi kutokana na hatua yake ya kulishutumu na kulionya jeshi dhidi ya kuchukua mamlaka nchini humo.
 
Back
Top Bottom