Sifahamu ni vipi jeshi litaendesha mambo, lakini nina matumaini. Kuna haja ya kuwepo wka uchaguzi kwa njia ya amani na jamii ya kimataifa kushirikishwa.
Bi Nandi-Ndaitwah ambaye pia anahudumu kama waziri wa mashauri ya nchi za kigeni, alinukuliwa akisema kuwa yale yanayoendelea katika taifa jirani wao la Zimbabwe yanaleta wasiwasi mkubwa.
Mwanasiasa huyo wa chama cha Movement for Democratic Change (MDC) amesema anafahamu kwamba Grace aliruhusiwa kuondoka nchini humo usiku wa kuamkia leo na jeshi.
Mwanasiasa huyo wa chama cha Movement for Democratic Change (MDC) amesema anafahamu kwamba Grace aliruhusiwa kuondoka nchini humo usiku wa kuamkia leo na jeshi.
Ameongeza kwamba alikuwa hana kwingi kwa kwenda kutafuta hifadhi baada yake kudaiwa kumdhalilisha mwanamitindo Afrika Kusini jambo lililomaanisha kwamba hawezi kuwa salama huko.
Hata hivyo, taarifa hizi hazijathibitishwa na jeshi.
Kwenye taarifa rasmi kwenye runinga ya taifa awali, Meja Jenerali Sibusiso Moyo alihakikishia taifa hilo kwamba rais na familia yake walikuwa salama na usalama wao ulikuwa umehakikishwa.
Nick Mangwana, mwakilishi wa chama tawala cha Zanu-PF nchini Uingereza ameambia BBC kwamba mwenyewe pia amepokea taarifa kwamba Grace hayupo tena nchini Zimbabwe.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.