Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Timu ya Barcelona Cadete B haijawahi kuifunga Espanyol Cadete A katika miaka michache ya mwanzo wa milenia mpya. Blaugrana walikuwa wakisaka mbinu, kwani hawakuwahi kuwafunga mahasimu wao ambao walikuwa imara zaidi kifiziki na uzoefu mwingi.
 
Lakini siku moja, historia ilibadilika. "Tulikwenda kwao na tulifunga tatu," Marc Valiente, beki ambaye yupo na KAS Eupen Ubelgiji na moja ya manahodha wa timu hiyo, ameikumbusha Goal. Ilikuwa ni 2002 na almasi mpya ya Barcelona ilikuwa Mwargentina mdogo mwenye umri wa miaka 14. Alifanya tofauti kubwa kwa timu isiyofungika.
 
Akitokea Rosario, aliwasili Barcelona na kuingia kwenye kikosi cha Infantil B (Infantil ni kundi la vijana wa umri chini ya miaka 12 kwenye soka la Kihispania), "aliingia kwenye chumba cha kubadilishia nguo bila hata ya kusema salamu", beki mwingine, Robert Franch, anakumbusha.
 
Kwenye timu ya vijana Barcelona, wachezaji wapya mara zote huulizwa swali moja linalofanana. "Unacheza wapi?," Rodolf Borrel alimuuliza Messi mbele ya timu yote Februari 2002. Bila ya kuinua kichwa chake, Leo alijibu kwa sauti ya chini. "Kama mshambuliaji".
 
Nilishangazwa naye," alisema Roger Gribet, ambaye alijiunga na Barcelona siku moja na Messi. "Nilipata ufahamu kwamba maendeleo yangu ya ukuaji yamefungua milango klabuni. Nilikuwa na urefu wa mita 1.70 katika umri wa miaka 12, lakini yeye hakuwa hata na mita 1.50," anaongea kwa mshangao mbele ya Goal, bado akishangaa, baada ya miaka 15.
 
Borrell aliwaeleza vijana kuwa Messi alikuwa namba 10 "ambaye aliwasili kutokea mbali" na alikuwa "mahususi sana", alisema Valiente ambaye aliongeza: "Basi siku hizo, hapakuwa na wachezaji waliotoka mbali kujiunga na La Masia". Messi alikuwa wa kipekee, hata kipindi hicho, na hapo bado wachezaji walikuwa hawajamwona na mpira mguuni.
 
Siku hiyo wachezaji hawakuona chochote kipya. "Tulielekezwa kucheza kwa kugusa mpira mara moja au mbili," Valiente anaeleza. "Katika umri mdogo tulifundishwa kumiliki mpira na kupiga pasi, kwa hiyo mpira ulikwenda kwa kasi. Lakini kwa ghafla hapa yupo kijana anayeweza kuugusa mpira mara nne au tano kwa kasi sawa ilitulazimu kufanya hivyo."
 
Lakini pamoja na yote bado walitaka kuyashuhudia kwenye mechi. Na Albert Benaiges, gwiji mkuu wa maendeleo ya soka katika Barcelona kwa zaidi ya miongo miwili, alikumbushia kitabu chake, Libero: "Tulilazimika kufanya haraka, kwani kama asingecheza mechi hizo mbili, asingeweza kucheza kwenye ngazi ya taifa hadi atimize miaka 18."
 
Mechi yake ya kwanza ilikuwa Machi 7, 2001 dhidi ya Amposta na alifunga goli. Hata hivyo maendeleo yake yaliingia dosari wiki moja baadaye kwani alivunjika mfupa wa mguu fibula ugenini dhidi ya Tortosa. Hadi leo hiii ni jeraha pekee la mfupa alilowahi kupata. Lakini katika umri huo, kengele za Barcelona zilikuwa zikigonga kwamba wamepata chombo. Messi hakucheza kwenye timu ya Infantil B tena.
 
Alipopona majeraha, alianza kucheza timu ya Infantil A na hakuwa na matatizo ya majeraha. Hapo napo tena alicheza mechi muhimu kwa sababu Borrell na Benaiges walimpandisha Cadete B (Umri chini ya miaka 16) mnamo 2002. Ni katika kundi hilo ambako aliweka lama hasa. Kwani alikuwa akicheza kwa kasi ya ajabu na ilikuwa vigumu kumkaba, hata wachezaji wenzake kwenye mazeozi.
 
Robert anaeleza kuwa "unaweza kumkimbiza kwa lengo la kumkata chini, lakini atakuwa ameshakuacha mbali na alikuwa akimpita beki mwingine". Anaongeza: "Alikuwa mashine na daima alikuwa mazoezini, kwa mbinu zake na aliweza kupata mpira kwa haraka mchezoni." Yeye na mabeki wengine wa kati walikuwa hawapendi kukabiliana naye mazoezini. "Kwa sababu tulijua kwamba hatuwezi kuunusa mpira ukiwa miguuni mwa Messi, hata ufanyeje."
 
Pamoja na yote hayo, bado alihifadhiwa sana. Hadi timu ilipokwenda Venice kucheza michuano na hapo ndipo Messi alipovunja barafu. "Alianza kufanya utani wake wa kwanza," Valiente anakumbusha. "Alikuwa na aibu kiasi kwamba hakuwahi kuongea na mtu kabla ya hapo." Alianza urafiki na Victor Vazquez, mmoja wa vito vya La Masia na rafiki mkubwa wa Mwargentina huyo kwenye timu ya vijana. Walikuwa pia wakisoma darasa moja.
 
Ilikuwa katika Venice ambako wachezaji wenzake walianza kumuita "enano" (mbilikimo). "Pamoja na kwamba tulianza kumuita hivyo siku nyingi, hatukufanya hivyo hadi tulipokuwa sote tunajiamini katika safari ya Venice," Roger Giribet, straika anaeleza. "Hata alipocheza kwa mara ya kwanza kwenye timu kubwa, alikuja kutuona La Masia na tulimuuliza: 'enano, umewezaje kucheza na watu wakubwa? na tuliangua kicheko.
 
Back
Top Bottom