Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kizazi cha 1987 kilihitimu Cadete A karibia wote kwa pamoja 2002-03 walifahamika kama timu bora sana La Masia, wakifanya kazi na marehemu Tito Vilanova na Alex Garcia. Hata hivyo hakuna kinachodumu milele na mwisho wa msimu, Cesc aliondoka kujiunga na Arsenal, na mwaka mmoja baadaye Gerard Pique alitua Manchester United.
 
Kwa upande wake Messi aliendelea kusonga mbele kutoka Jevenil A (chini ya miaka 19) hadi Barcelona C (ambayo haipo tena) kisha Barcelona B, kwa mwaka mzima. Katika umri wa miaka 16, alianza kucheza timu kubwa na katika umri wa miaka 17 tayari alikuwa mchezaji kamili wa timu kuu, chini ya mbawa za Ronaldinho, mchezaji bora wa dunia wa kipindi hicho.
 
Giribet anaamini Messi tofauti na wachezaji wengine haathiriwi na presha. "Hajui presha ni nini," aliielezea Goal. "Kuna wachezaji wengi wenye kipaji ambao hawafanikiwi kwa sababu hawawezi kukabiliana na presha. Miguu yangu ilikuwa ikigongana nilipokuwa nikicheza mbele ya watu 1,500 naye anacheza sawa sawa, iwe kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa au bustanini."
 
Valiente anakiri. "Wale tunaomfahamu hatukushangazwa kuona akicheza kikosi cha kwanza timu ya wakubwa katika umri mdogo, lakini namna alivyofanikiwa kuzoea kwa haraka kila hatua ya maendeleo yake," aliema. Na Torras anaongeza: "Ni mchezaji asiyezuilika mara zote na hapakuwa na kanuni ya kumzuia."
 
3661f063eb3174a601c3e0f5f7d8bd2e.jpg
Ni ya Zaidi ya ukweli!
 
Back
Top Bottom