Hapa nimezingatia mambo matatu. Mosi kuheshimu na kabla ya kutumia kuomba ruhusa. Pili ni kutokuomba lakini kujiweka katika utayari wa kulipa fidia endapo shauri litafikishwa panapohusika na mwisho kuangalia ukomo wa kitambo cha uhai wa sheria ya hakimiliki.
Kifaa hiki huweza kuzalisha sampuli mbalimbali za milio ya kila kifaa cha muziki baada ya utunzi ambao ulitumia sampuli ya mapito ya mapulizo ya saxophone kama ile ya bendi ya Juwata Jazz Band katijka wimbo wake wa ajali ambayo imeamsha limeamsha suala la kisheria juu ya hakimiliki dhidi ya wimbo wa WCB maarufu kama Zilipendwa.
Utayari wetu kuheshimu ubunifu wa wengine na kuomba ridhaa au ruhusa rasmi kwa makubaliano katika kutumia sehemu ya ubunifu wa wengine katika kazi zetu.
Lipo suala adhimu la mmiliki halali wa wimbo. Inafahamika vyema bendi maarufu ya Juwata Jazz Band kwamba enzi hizo jumuiya ya wafanyakazi ikiwa moja ya matawi tano muhimu ya CCM iliasisi uundwaji na ulezi wa bendi baadae ikawa imebadili jina na kuitwa Ottu Jazz Band
na hatimaye sasa baada ya kukabidhiwa rasmi kwa wanamuziki wenyewe kuiendesha inaitwa Msondo Ngoma. Kimantiki mabadiliko ya majina yanaleta dosari katika madai ijapokuwa uhalali ungalipo kama miliki halali.