Mwaka 1994 alipata fedha akanunua nyumba kwa mtu aliyemtaja kuwa ni Paulo Kihampa, baada ya kujiridhisha kwa kutumia kiogozi wa Serikali ya Mtaa Stop Over, Abuu Mbasi kuwa haiko ndani ya hifadhi ya barabara.
Nilinunua nyumba kwa bei ya Sh2 milioni. Baada ya hapo nikajenga nyumba ya ghorofa moja na baada ya miaka mitano aliongeza nyingine ya gorofa moja.” anasema.
Nilikaa miaka miwili nikaanza kujenga taratibu nyumba ya tatu ambayo haikuwa ya ghorofa, nilitumia miaka mitatu kukamilisha ujenzi huo nikiwa bado na kazi yangu ya udereva,” anasema.
Nilipokamilisha tu nikaanza tena kujenga nyumba ya nne ambayo pia niliijenga kidogokidogo mpaka sasa kiwanja chake kilikuwa na nyumba nne ndani ya eneo moja,” anasema.
“Najiuliza sijui kwanini bado naishi hapa, lakini sipati jibu. Nikilala nikiamka najikuta nipo hapa,” anasema Leo ambaye licha ya nyumba yake kubomolewa bado anaendelea kuishi katika mabaki ya nyumba yake.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.