Uongozi wa klabu ya Yanga imesema bado unafikiria kumruhusu kwa mkopo mshambuliaji wake Matheo Anthon kujiunga na timu ya Lipuli FC, ambayo imeonyesha nia ya kumuhitaji kwa ajili ya kuimarisha safu yake ya ushambuliaji kwenye mechi zilizopita.
Msemaji wa Yanga Dismas Ten, ameiambia Goal, mpaka sasa kocha wao hajawapa majibu yoyote kuhusiana na mchezaji huyo kutakiwa na Lipuli, na wao hawawezi kufanya chochote wakisubiri kauli yake.
George Lwandamina ndiyo kocha mwenye kujua mapungufu ya timu yake na mahitaji hivyo sisi kama watendaji tumemfikishia mezani kwake na yeye ndiyo mwenye maamuzi ya kumruhusu au kumzuia Matheo kwenda Lipili FC," amesema Ten.

Msemaji huyo pamoja na kukiri kuwa nikweli mshambuliaji huyo anasota benchi lakini amesema endapo kocha atamruhusu wapo tayari kumpa baraka zote na wataitaka Lipuli kumtumia mchezaji huyo kwenye kikosi cha kwanza ili kumpa nafasi ya kupandisha kiwango chake.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.