Mafuta: Mafuta ni moja ya virutubishi vitatu vinavyohitajika kwa wingi na mwili, bila mafuta mwili hauwezi kuishi. Pamoja na kutoa kalori 9 kwa kila gramu, mafuta husaidia kuupa mwili joto wakati wa baridi. Mafuta pia hulainisha maungio ya mifupa. Mafuta hutunza baadhi ya vitamini kama A, D, E na K