Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

JINSI YAKUANDA NA KUPIKA NDIZI MBIVU NA NAZI . Ndizi mbivu za kupika 10 Nazi kavu 3 Sukari kiasi Hiliki kiasi 1 Zipasue ndizi katikati kwa marefu, uzitoe moyo wake. 2 Zimenye kisha maganda uyaoshe. Yapange vizuri maganda hayo ndani ya sufuria safi (kwa chini). Chukua vipande vya ndizi uvipange juu ya maganda.(ndizi ziweke chali, usizifudikize). 3 Kuna nazi uchuje tui zito mbali na jepesi mbali. Chukua tui jepesi ulitie katika ndizi kisha uziteleke. Zipike mpaka tui likauke na ndizi ziive. Nyunyuzia sukari kidogo. Twanga hiliki utie juu yake. Chukua lile tui zito ulimimine uache liwe linatokota kwa moto mdogo sana. Tui likikauka na kutoa mafuta epua na uziache zipoe. Unapopakua, zitoe taratibu bila ya kuzivuruga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…