Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mkuu asante sana, karibu sana hapa na endelea kutumwagia elimu hiyo ya afya ya mwili. Karibu sana mkuu
 
Sababu Hatarishi Kwa Mtu Kupata Maambukizi katika njia ya mkojo (U.T.I)

1.JINSIA - Wanawake wapo katika hatari kubwa kupata U.T.I kuliko Wanaume, hii ni kutokana na maumbile ya via vya uzazi ambapo wanawake wana Urethra fupi hivyo kuwafanya Bakteria kusafiri kwa urahisi na uharaka na kufika kwenye Kibofu cha mkojo.

2.Baadhi ya njia za uzazi wa mpango, kama vile vitanzi.

3.Matatizo/DOSARI katika njia ya Mkojo - Matatizo haya yanaweza kuwa ya kuzaliwa nayo au yale yanayopatikana baada ya kuzaliwa, mfano kuziba kwa njia ya mkojo.

4.Matumizi ya muda mrefu ya mpira wa mkojo (Catheter)

5.Upungufu wa kinga Mwilini, hii hupelekea mwili kushindwa kupambana na vijidudu. Magojwa kama Kisukari, Saratani na Hata Matumizi ya Mionzi-Tiba kwa muda mrefu.

6.Ukomo wa Hedhi (MENOPAUSE), Kushuka kwa kiwango cha kichocheo (Hormone) aina ya Oestrogen Mara tu baada ya mwanamke kuanza kukosa kuona hedhi hupelekea kumuweka katika hatari ya kupata U.T.I
 
Aaaa jamanii[emoji134] [emoji134] [emoji134]
 
Dalili za Maambukizi katika njia ya Mkojo.

Zifuatazo ni baadhi ya dalili za U.T.I na mara uzionapo wahi kituo cha Huduma za afya mapema ili upate vipimo na tiba.

1.Maumivu wakati wa kukojoa, huanza taratibu lakini baadae huwa makali zaidi.

2.Uwepo wa damu katika mkojo.

3.Maumivu ya Tumbo, hasa chini ya kitovu mpaka kwenye kinena.

4.Kuhisi kama unaungua wakati wa mkojo unapopits kwenye Urethra (wakati wa kukojoa)

5.Homa Kali, Kichefuchefu na Kutapika.

6.Maumivu chini ya mgogo (karibu na kiuno) na pembeni juu ya kiuno.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…