Walimu 12 na mkurugenzi wa Shule ya Msingi Mount Pleasant iliyopo Tabata jijini Dar es Salaam, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka matano, likiwemo la kuishi nchini kinyume cha sheria.
Mwendesha mashtaka wa Uhamiaji, Gerald Maridai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Godfrey Mwambapa amedai washtakiwa hao isipokuwa mkurugenzi wa shule hiyo walijihusisha na kazi bila kibali halali.
Novemba 24,2017 washtakiwa wanadaiwa wakiwa raia wa Uganda walikutwa wakifanya kazi bila kuwa na leseni au vibali vinavyowaruhusu kufanya hivyo. Pia, wanadaiwa kuingia nchini bila ya kuwa na hati za utambulisho.
Nairobi-Kenya. Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan leo Jumanne Novemba 28, 2017 amemtembelea mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu aliyelazwa Hospitali ya Nairobi nchini hapa.
Lissu amelazwa hospitalini hapo akiuguza majeraha ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 aliposhambuliwa Septemba 7 akiwa nyumbani kwake, Area D mjini Dodoma.
Nairobi, Kenya. Kiongozi wa muungano wa upinzani wa Nasa, Raila Odinga amedai atakula kiapo kama “rais wa watu” Desemba 12.
Akiwahutubia wafuasi wake katika barabara ya Mayanja baada ya kutawanywa na polisi kwenye viwanja vya Jacaranda, alisema atatumia Ibara ya 1 kuapa inayosema mamlaka ya nchi yanatoka kwa watu.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.