Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Timu hii ya wataalamu inayoondoka kesho (leo) inajumuisha madaktari bingwa wanne wa magonjwa ya mfumo wa chakula na ini, wauguzi wawili wanaosimamia mifumo ya hadubini na mhandisi wa vifaa tiba anayesimamia mitambo ya hadubini,” alisema Aligaesha. Alisema mafunzo hayo yatachukua muda wa miezi mitatu na wanatarajiwa kurejea nchini wiki ya kwanza ya Machi 2018.
 
Aligaesha alisema ni matarajio yao kwamba wataalamu hao watakaporudi wataongeza ufanisi katika kufanya uchunguzi na tiba ya magonjwa ya ini kwa kutoa mawe, kuzibua mifereji ya nyongo na kongosho iliyozibwa na uvimbe.
 
Tutaweza kufanya upasuaji wa ini kuondoa uvimbe mkubwa unaoodhofisha afya na kutishia maisha ya wagonjwa. Aidha lengo kubwa ni kujenga uwezo wa ndani kwa muda mfupi utakaowezesha kufanyika kwa upandikizaji wa ini kwa wagonjwa wenye mahitaji,” alisema Aligaesha.
 
Hata hivyo, alisema gharama za kutibu ini au upandikizaji ni zaidi ya Sh100 milioni nchini India, hivyo huduma hiyo ikianza kutolewa hapa nchini itapunguza nusu ya gharama. “Tulikuwa tunawahudumia mpaka wanapofariki, hatukuwa na morari ya kuwapeleka nje kwani kupandikiza ini si kwa hatua za mwisho, bali kwa hatua za awali za ugonjwa, hivyo tukikamilisha utaalamu huu tutawatafuta katika hatua za awali na kuzuia uharibifu wa ini zaidi kwa kuwafanyia upasuaji au kupandikiza ini,” alisema Dk Rwegasha.
 
Kwa kuwa tumepanua huduma zetu za uchunguzi, tutaanza sasa kutoa tiba kwa kumsaidia mgonjwa kutoa uvimbe au kufanya upandikizaji wa ini jingine kama ugonjwa unagundulika kwa hatua za mwanzo, miundombinu ipo kwa sasa na tuna vyumba vya upasuaji na ICU za kutosha,” alisema Dk Mwanga.
 
Kampuni ya uendeshaji wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kadco), inatarajia kulipa fidia ya Sh400 milioni kwa familia 429 zilizofanyiwa tathmini mwaka 2002 kwa ajili ya kupisha upanuzi wa uwanja.

Pia, wananchi hao watakaolipwa watatakiwa kuondoka eneo hilo kupisha upanuzi zaidi wa uwanja huo.
 
Hayo yalisemwa juzi na naibu waziri wa uchukuzi na mawasiliano Wizara ya Ujenzi, Atashasta Nditiye wakati akizungumza na uongozi wa uwanja huo.

Alisema baada ya kutembelea uwanja huo na kuzungumza na uongozi, amebaini kuwapo kwa changamoto hiyo ya kulipwa fidia kwa wananchi hao ambao wamefanyiwa tathmini huku kukiwa na wananchi ambao hawakufanyiwa tathmini wakihitaji nao kulipwa.
 
Kwa waliokuja baada ya tathmini hao ni wavamizi na hatutawalipa chochote, naomba waelewe hilo. Kumekuwapo na changamoto ya wananchi waliokuja baada ya tathmini kuhitaji nao kulipwa fidia jambo ambalo haliwezekani kabisa na Serikali inatafuta fedha kwa ajili ya familia 429 tu si vinginevyo.’’
 
Kwa waliokuja baada ya tathmini hao ni wavamizi na hatutawalipa chochote, naomba waelewe hilo. Kumekuwapo na changamoto ya wananchi waliokuja baada ya tathmini kuhitaji nao kulipwa fidia jambo ambalo haliwezekani kabisa na Serikali inatafuta fedha kwa ajili ya familia 429 tu si vinginevyo.’’
 
Alisema Serikali inataka kupanua uwanja huo na kujenga miradi mbalimbali, ikiwamo maduka na maeneo mbalimbali ya kupumzikia ili kuwawezesha wageni wanaofikia uwanjani hapo kupumzika badala ya kwenda mjini.

Naye mwenyekiti wa bodi ya uwanja wa Kia, Gregory Teu alisema kuwa, hivi sasa Serikali inatafuta fedha kwa ajili ya kuwalipa fidia wananchi hao waliofanyiwa tathmini, hivyo kuwataka ambao hawajafanyiwa tathmini kuondoka wenyewe kupisha shughuli za upanuzi wa uwanja huo.
 
Awali, akitoa taarifa kaimu mkurugenzi wa Kadco, Ande Mukoma aliwataka wananchi hao kusikiliza maagizo ya Serikali inavyowaelekeza.

Mukoma alisema watakaolipwa ni wale waliofanyiwa tathmini tu, hivyo wengine kuanza kutafuta namna nyingine kabla shughuli za upanuzi wa uwanja huo hazijaanza.
 
Mitambo

Upanuzi wa Kia unatarajiwa kuongeza idadi ya abiria wanaotumia uwanja huo kufikia zaidi ya milioni moja na ndege 11 zinataweza kutua kwa wakati mmoja.

Pia, inaelezwa kuwa kufungwa kwa mashine za ukaguzi kusaidia kupunguza matukio ya upitishaji wa dawa za kulevya na utoroshaji wa nyara za Serikali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…