Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

%E2%80%AA%2B255+785+434+419%E2%80%AC+20171130_145559.jpg
 
Tukio hilo lilitokea jana saa 6 mchana wakati wanakijiji hao walipokuwa wanaenda kuzika na ndipo ghafla mvua kubwa iliyoambatana na radi na upepo mkali ilipoanza kunyesha kitu ambacho kiliwafanya waombolezaji kukimbia majumbani mwao kwa kuhofia kupigwa na radi.
 
Hata hivyo, Baadhi ya wananchi walivumilia nakurejea na jeneza lililokuwa na mwili wa marehemu nyumbani na kuahilisha maziko kwa muda ili kupisha hali hiyo itulie na walikwenda kuzika baadaye katika makaburi yaliyopo kijijini hapo.
 
Mwenyekiti wa serikali ya kitongoji cha Kaungo, Robert Kanoni, akizungumzia tukio hilo amesema wananchi wakiwa wanaelekea kufanya maziko ya marehemu aliyetambulika kwa jina la Dismas Kanoni, ghafla mvua kubwa iliyoambatana na radi na upepo mkali ilianza hali iliyosababisha waombolezaji kuingiwa na hofu.
 
Bw. Kanoni amesema tukio hilo lilizua hisia za kishirikina kwa wananchi wa kijiji hicho kwani miezi miwili iliyopita baba yake na marehemu huyo alifariki baada ya kugongwa na gari la kampuni ya ujenzi wa barabara na walipofanya maziko siku iliyofuata walikuta ngozi ya kondoo juu ya kaburi la marehemu kitendo kilichowashangaza.
 
Back
Top Bottom