Kuku wa kuchoma Mahitaji Kuku mzima Kitunguu saumu 1 tsp Tangawizi 1 tsp Limao Binzari ya manjano 1/2 tsp Garam masala 1/2 tsp Curry powder 1/2 tsp Chumvi Mafuta vijiko 2 Njia Chukuwa kuku muweke mahitaji yote kitunguu saumu, tangawizi,limao,binzari ya manjano,garam masala,curry powder,chumvi na mafuta na mpake hakikisha anaingia vizuri kwy kuku na kisha muweke kwy friji chini kwa muda wa saa 6 au hata usiku mzima Kisha washa oven 200°c na muweke kuku wako kwa muda wa saa 1 kisha mpasue katika ili kumfungua ili achomeeke vizuri kwa ndani kwa muda wa dk 35 na tayari na hakikisha anapata yangi nzuri ya kahawia. Enjoy unaweza kula na chochote ni mtamu sana