Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

EASY CHOCOLATE CAKE MAHITAJI Unga wa ngano 1 1/2 cups (190g) Sukari 1 cup (200g) Cocoa powder 1/4 cup Siagi (butter) 3/4 cup (75g) yayusha Maji (warm) 1 cup (240ml) Vanilla 1 tsp Baking powder 1 tsp Baking soda 3/4tsp Chumvi 1/4 tsp Limau (fresh lemon juice) 1tbsp JINSI YA KUTENGENEZA Tayarisha treya kwa kupaka siagi (unaweza kutumia sufuria pia) Changanya unga, sukari , cocoa powder, b.powder, b.soda na chumvi mix vizuri mpaka vichanganyike Changanya maji, vanilla, limau na siagi (iliyoyayushwa iwe warm kidogo) Mimina kwenye ule mchanganyiko wa unga changanya vizuri sana mpaka vichanganyike uwe hauna madonge Mimina kwenye treya weka kwenye oven 180°c kwa 30-35 min Unaweza kueka chokolate juu au kula bila chokolate Jinsi ya kutengeneza chocolate ya kueka juu ipo kwenye pic zetu pia unaweza kuweka chocolate spread
 
BBQ CHICKEN STEWERS (MISHKAKI YA KUKU) MAHITAJI Kidari cha kuku (chicken breast) 1/2 kg Tangawizi ilosagwa 1 tsp Kitunguu saum 1tsp Pilipili ilosagwa kiasi Chumvi kiasi Limau (lemon juice) 1tbsp Tandoori masala 1tsp Bizari nyembamba (cumin powder) 1tsp Bizari manjano 1/2 tsp Pilipili manga (black paper powder) 1/2tsp Rangi ya orange (food colour) 1/2 tsp Soy sauce 1tbsp Mafuta 2tbsp JINSI YA KUTENGENEZA Mkate kuku vipande vidogo kiasi mkoshe Changanya vitu vyote kwenye chombo than mtie kuku umchanganye vizuri mfunike mueke pembeni kwa masaa 3 au zaidi Weka kwenye vijiti kama unavyoona kwenye pic Choma kwa grill uwe unamgeuza mpaka awive Enjoy kwa chips,wali or anything
 
MKATE WA MAYAI MAHITAJI Mayai (eggs) 1 mug Unga wa ngano (plain flour) 1 mug Sukari (sugar) 3/4 mug Hiliki 1 tsp Baking powder 1/2 tsp JINSI YA KUTENGENEZA Washa oven 160°c Ipake mafuta pan ya kuchomea (sufuria) weka pembeni Changa unga na baking powder uchunge kwa chungio weka pembeni Saga mayai sukari, hiliki kwa hand mixer sana mpaka yavimbe na yawe fluffy about 20mins (kila ukisaga sana mkate unatoka laini zaidi na mzuri zaidi) Than tia unga uchanganye kwa mwiko or spatula changanya vizuri ili unga uchanganyike ila usichanganye sana ili mayai yasirudi (dont over mix) Mimina kwenye pan yako ulopaka mafuta weka kwenye oven choma kwa nusu saa au zaidi mpaka ukitia kijiti kitoke kilavu Note Usiutowe kwenye oven kuuangalia mpaka at least after 25mins Enjoy na coffee
 
MKATE WA MAYAI MAHITAJI Mayai (eggs) 1 mug Unga wa ngano (plain flour) 1 mug Sukari (sugar) 3/4 mug Hiliki 1 tsp Baking powder 1/2 tsp JINSI YA KUTENGENEZA Washa oven 160°c Ipake mafuta pan ya kuchomea (sufuria) weka pembeni Changa unga na baking powder uchunge kwa chungio weka pembeni Saga mayai sukari, hiliki kwa hand mixer sana mpaka yavimbe na yawe fluffy about 20mins (kila ukisaga sana mkate unatoka laini zaidi na mzuri zaidi) Than tia unga uchanganye kwa mwiko or spatula changanya vizuri ili unga uchanganyike ila usichanganye sana ili mayai yasirudi (dont over mix) Mimina kwenye pan yako ulopaka mafuta weka kwenye oven choma kwa nusu saa au zaidi mpaka ukitia kijiti kitoke kilavu Note Usiutowe kwenye oven kuuangalia mpaka at least after 25mins Enjoy na coffee
 
MAANDAZI YA CUSTARD MAHITAJI unga wa ngano 1/2 kg Hamira 2 tsp Sukari 100 gm Maziwa ya maji 100ml Chumvi 1/2 tsp Maji 1/2 kikombe Yai 1 Butter 100gm Unga wa Custard 2tblsp Mafuta ya kupikia MATAYARISHO Changanya unga wa ngano, unga wa custard, hamira (hamira unaweza kuiroweka kabla ya kuchanganya) chumvi, sukari na butter pamoja mpaka ichanganike vizuri. Piga yai na maziwa pamoja mpaka yai lichanganyike na maziwa. Halafu tia kwenye unga changanya. Tia maji kidogo kidogo mpaka uwe donge laini. Si lazima utumie maji yote na kama kidogo ongeza. Ukande unga kwa dakika 15. Ufunike uwache uumuke. Ukiwa tayari kata size unopenda. Yaweke tena yaumuke. Halafu choma kwa mafuta. Yakiiva yachuje mafuta yaache yapowe. Ukipenda saga sukari unyunyize juu yake. Tayari kwa kuliwa na chai ya maziwa. Yaani ni matamu sana.
 
MISHKAKI YA NYAMA MAHITAJI Nyama 3/4 kg Chumvi kiasi Limau 1 (lemon) Soy souce 1 tbsp Bizari nzima (cumin seeds) 1tbsp Pilipili manga (black paper) 1/2 tsp Tangawizi 1tsp (ginger paste) Kitinguu saum 1tsp (garlic paste) Mafuta ya kupikia 2tbsp Pilipili ilosagwa (ukipenda) JINSI YA KUTENGENEZA Weka bizari nzima kwenye pan weka kwenye moto ikipata moto kidogo itowe uitwange Changanya vitu vyote pamoja than weka chops Funika weka kwa masaa 4 ikolee vizuri Chomeka nyama kwenye vijiti Weka kwenye trayer tia kwenye grill igeuze geuze kila wakati ili iwive vizuri Enjoy
 
VEGETABLE FRIED RICE MAHITAJI Mchele 1/2 kg Mix vagetable 1 cup Chumvi kiasi Mafuta 3 tbsp Soy source kiasi Kitunguu maji 1 cha kiasi (kikate kama cha sambusa) Kitunguu saumu tembe 1 JINSI YA KUTENGENEZA Kwanza chemsha wali wako kama kawaida uwive lakini usivurugike ukisha kuuchuja maji uweke pembeni Kwenye sufuria ya kupikia weka mafuta 3 tbsp weka kitunguu maji changanya mpk kilainike kisipige rangi weka kitunguu saumu iloparwa changanya vizuri Sasa weka mix vegetable zako changanya na vitunguu maji mpaka vikaangike weka chumvi kidoogo Sasa weka wali wako ulochemsha mwagia juu soy source changanya vizuuri na wali wako utakuwa tayari kwa kuliwa ENJOY
 
NYAMA YA KUCHOMA (GRILLED CHOPS) MAHITAJI Chops vipande 10 (10 pieces) Chumvi kiasi Limau 1 (lemon) Soy souce 1 tbsp Bizari nzima (cumin seeds) 1tbsp Pilipili manga (black paper) 1/2 tsp Tangawizi 1tsp (ginger paste) Kitinguu saum 1tsp (garlic paste) Mafuta ya kupikia 2tbsp Pilipili ilosagwa (ukipenda) JINSI YA KUTENGENEZA Weka bizari nzima kwenye pan weka kwenye moto ikipata moto kidogo itowe uitwange Changanya vitu vyote pamoja than weka chops Funika weka kwa masaa 4 ikolee vizuri Weka kwenye trayer tia kwenye grill mpaka iwive uigeuze pande zote mbili Enjoy
 
CHOCOLATE CAKE MAHITAJI Unga 2 cups Sukari 1 3/4 cup ( nimetumia icing sugar) Cocoa powder 3 tbsp Drinking chocolate powder 4 tbsp Baking powder 1 tbsp Mayai 5 Siagi 1 cup Maziwa 1 1/4 cup Vanila 1 tbsp ( unaweza kutumia esse JINSI YA KUTENGENEZA Kwanza washa oven lako moto 180 Changanya unga , baking powder , cocoa powder na chocolate drinking powder vizuri weka pembeni Kwenye bakuli la kusagia cake weka siagi na sukari saga kwa mashine mpk iwe cream weka yai moja moja huku unasaga kwa mashine (HAPA HAKIKISHA UNASAGA SANA ILI CAKE YAKO ISIWE NA HARUFU YA MAYAI) Sasa weka unga na maziwa kwa matabaka matatu ( NAKUSUDIA ANZA KUWEKA MAZIWA KIDOGO THAN UNGA KIDOGO, MAZIWA UNGA, MAZIWA TENA MALIZIA NA UNGA ) kila ukiweka uwe unachanganya kwa mashine yako weka vanila yako Baadae paka siagi treya yako ya kuchomea mimina mchanganyiko wako weka kwenye oven kwa muda wa dakika 30 mpka 40 au mpk iwive ENJOY
 
FRUITS ICE LOLLY MAHITAJI Strawberry kiasi Mango (embe mbivu ) kiasi Sukari kiasi JINSI YA KUTENGENEZA Saga strawberry zako kwa blender weka kwenye kibakuli weka sukari kiasi unayopenda changanya vizuri kama hupendi kuweka sukari sio lazima Anza kuweka kwenye vikopo vyako kila kikopo nusu than weka kwa frizer kwa muda wa saa moja au hata zaid sio mbaya Baadae toa saga embe lako kwa blender jalizia kwenye vikopo vyako nafasi ilobaki chomeka vijiti vyako weka kwenye frizer mpk zigande tayari kwa kuliwa ENJOY (UNAWEZA KUTUMIA FRUITS UNAZOPENDA
 
Back
Top Bottom