Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola amesema anajutia sana mazungumzo ambayo alifanya na mchezaji wa Southampton Nathan Redmond punde baada ya mechi yao kumalizika Jumatano.
City walishinda 2-1.
Guardiola, ambaye aliingia uwanjani na kuzungumza na winga huyo, ametakiwa kufafanua kuhusu kitendo hicho chake na Chama cha Soka cha England.
Redmond amesema Mhispania huyo alikuwa tu anamsifia.
Ijumaa, Guardiola alisema: "Siwezi kujidhibiti. Natumai nitaweza kufanya hivyo, natumai naweza kuimarika."
 
Meneja huyo wa zamani wa Barcelona na Bayern Munich amepewa hadi Jumatatu kutoa ufafanuzi.
"Kile Redmond alichosema ndicho hicho, navutiwa naye kama mchezaji na namshukuru kwa aliyoyasema," amesema.
"Iwapo FA wanataka taarifa yangu tena, ninaweza kufafanua chochote wanachotaka nifafanue. Ikiwa hawaniamini, sijui nafanya nini hapa."
Guardiola alimwendea Redmond muda baada ya Raheem Sterling kufunga bao la ushindi la City dakika ya 96 uwanjani Etihad.
Alianza kusema kwa sauti na kuashiria kwa mikono yake, huku Redmond akionekana kufunika mdomo wake na kumjibu.
 
MAN UTD YAMTOLEA MACHO CRISTANTE


Manchester United inataka kumsajili kiungo wa Atalanta, Bryan Cristante kuwa mrithi wa Marouane Fellaini, kwa mujibu wa The Sun .
Mashetani Wekundu wapo tayari kumpoteza Fellaini na kiwango cha Cristante akicheza kwa mkopo Serie A kimemshawishi Mourinnho kuamini kuwa mchezaji huyo ni mbadala sahihi kwa Fellaini.
Atalanta wana uwezo wa kumsajili Cristante kutoka klabu yake mama Benfica kwa paundi milioni 10 mwisho wa msimu, na kisha kumuuza kiungo huyo Man United kwa paundi milioni 31.
 
ARSENAL NA MAN CITY ZAMWANIA EVANS


Beki wa kati wa West Brom Jonny Evans amezivutia Manchester City na Arsenal kwa ajili ya uhamisho wa Januari, kwa mujibu wa The Telegraph .
Ilitipotiwa kuwa ofa ya Arsenal ya £25 milioni ilikataliwa Agosti 31 kwa ajili ya mchezaji huyo, kwani WBA wanataka kiasi kisichopungua £30m.
 
MADRID KUMSAJILI VINICIUS 2018


Real Madrid watakamilisha usajili wa kinda wa Kibrazili Vinicius Junior msimu ujao wa majira ya joto, kwa mujibu wa AS .
Madrid walikubali dili la €45 milioni kwa ajili ya Vinicius wa Flamengo mwezi Mei, lakini mshambuliaji huyo hawezi kuruhusiwa kuhama hadi atakapotimiza umri wa miaka 18 Julai mwakani.
 
COUTINHO KULIPWA €14M KWA MWAKA BARCA


Barcelona watampa Philippe Coutinho mkataba wenye thamani ya €14 milioni kwa msimu ikiwa watafanikiwa kuishawishi Liverpool kumuuza Mbrazili huyo, kimedai Sport .
Liverpool walikataa ofa zote kwa ajili ya Coutinho majira ya joto, lakini Barca wanataka kurudi upya Januari na wapo tayari kutoa ofa ya €150m kwa ajili ya kiungo huyo.
 
880f559356ab7862067a9d3d68e246f6.jpg
 
Back
Top Bottom