Sijui ni mende wangapi hutumiwa hadi upate kikombe cha chai, lakini wakazi wa New Orleans wana imani sana na tiba hii,” aliandika.
Leo katika hospitali Uchina, krimu inayotengenezwa kwa kutumia ungaunga wa mende waliosiagwa hutumiwa kutibu vidonda vya moto na pia humezwa kutibu vidonda vya tumbo.
Mende wanahitajika sana hivi kwamba Wang Fuming aliamua kufungua biashara ya ufugaji mende eneo la Shandong, mashariki mwa Uchina. Huwa anafuga mende 22 milioni kwa wakati mmoja. Anasema tangu 2010, bei ya mende waliokaushwa imepanda mara kumi.