Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Nasisitiza juu ya kukutana na watu wapya, kwa sababu nimegundua ya biashara nyingi zimekuwa hazifanyi vizuri kwa sababu zimekuwa na watu ambao wanaizunguka biashara ile ni wale wale kila siku. Hivyo kila siku fanya tathimini juu wateja wapya ambao wamekuja katika biashara yako.
 
Katika makala yetu ya leo nitaomba tu nikukumbushe mambo ambayo unatakiwa uyakumbuke kila wakati kwenye maisha yako . Ni mambo ya msingi kwani yatakusaidia kuweza kuwa na mtazamo chanya na kubadili mambo mengi sana kwako.
 
1. Mambo yaliyopita hayawezi kubadilishwa tena.
Unatakiwa kuelewa kama kuna mambo ambayo yameshapita huwezi kuyabadilisha tena hata kama yalikuumiza au ulifanya makosa kiasi gani. Kwa sasa unatakiwa kuganga yajayo, habari ya mambo yaliyopita yatumie kama fundisho tu kwako, lakini ndio yameshapita, usiumize kichwa na kujilaumu sana.
 
2. Maoni ya watu hayaamui hatima ya maisha yako.
Hata siku moja usije ukakaa ukafikiri kwamba maoni ya watu wengine wanayosema juu ya wewe ndiyo yanaamua maisha yako yawe vipi. Maisha yako yanabaki hivyo yalivyo kwa sababu wewe umeamua yawe hivyo. Lakini usikubali hata siku moja maoni ya watu yakurudishe nyuma na usiyatumie kama kisingizio.
 
3. Maisha yako yatakuwa mazuri tu ukijipa muda.
Ukiamua siku zote kubadilisha maisha yako unaweza. Kikubwa jipe muda wa kutosha kubadilisha maisha yako hatua kwa hatua na kila kitu kitabadalika. Haijalishi unaona maisha yako ni magumu kiasi gani, lakini muda ndio kila kitu. Muda unaweza kusawazisha mambo mabaya na yakawa mazuri kabisa. Tumia muda wako vizuri.
 
4. Utashindwa tu, kama utakata tamaa.
Ndoto yoyote ile uliyonayo au ambayo unatamani kuifikia una uwezo mkubwa wa kuifikia. Ila hautaweza kuifikia ndoto yako hiyo ikiwa utafika mahali wewe mwenyewe utaamua kukata tamaa. Moja ya sumu kubwa ya kimafanikio ni kukata tamaa, ukikata tamaa ujue kila kitu kwako kimeishia hapo na hutaweza kusogea tena
 
5. Furaha ya kweli inapatikana ndani mwako.
Ukweli huu hautakaa ubadilike kamwe kwamba furaha ya kweli inapatikana ndani mwako na wala si nje yako. Unaweza ukakazana sana kutafuta furaha nje kwa kufanya vitu ambavyo unaamini vitakupa furaha, lakini ukivipata vitu hivyo unashangaa ile furaha tena bado huna. Hivyo jifunze kutafuta furaha ya kweli ndani mwako.
 
6. Mawazo chanya, ni njia ya mabadiliko chanya pia.
Mbinu mojawapo ya kuwa na maisha bora. Ni kwa wewe kuwa na mawazo chanya. Unapokuwa na mawazo chanya ni rahisi sana kwa wewe kuweza kuleta mabadiliko chanya pia. Watu wengi wanashindwa kwa sababu ya kuwa na mlundikano wa mawazo mengi ambayo kwao ni hasi. Kuwa na mawazo chanya ubadili maisha yako.
 
Kuna wakati mwingine Katika maisha yetu ya kila siku tunasema pesa ndo kila kitu.Ni kweli lakini kuwa na pesa bila wazo mahususi katika matumizi ni sawa na kuzima moto kwa chafya. Unashangaa huo ndo ukweli watu wengi tunapata pesa lakini hatujui tuitumie vipi pesa hiyo ili iweze kujisalisha. zipo sababu nyingi ambazo zinasababisha matumizi mabaya ya fedha.
 
Pesa hii ina majina mengi hii ni kutokana na mahali husika wapo wanaita pesa ni sababuni ya roho, mtonyo, mapene, ankara na majina mengine mengi. Leo katika makala haya nitakwenda kukuelezea juu ya matumizi mabaya ya pesa yanayofanya kila siku tuwe katika hali ya umaskini.
Yafuatayo ndiyo matumizi mabaya ya pesa.
 
Pesa hii ina majina mengi hii ni kutokana na mahali husika wapo wanaita pesa ni sababuni ya roho, mtonyo, mapene, ankara na majina mengine mengi. Leo katika makala haya nitakwenda kukuelezea juu ya matumizi mabaya ya pesa yanayofanya kila siku tuwe katika hali ya umaskini.
Yafuatayo ndiyo matumizi mabaya ya pesa.
 
Kutokuwa na mpangilio wa matumizi ya pesa.
Moja ya changamoto kubwa inayowakumba wengi wetu ni kwamba hatuana mapangalio sahihi juu ya matumizi ya fedha. Tupo baadhi yetu ambao hutamani kila kitu ambacho tunakiona mbele yetu na kukinunua hata kama ulikuwa hauna mapngo wa kununua kitu hicho. Tupo baadhi yetu tukiwa tunatembea tukiona hiki na kile ni lazima tununue hiyo siyo nidhamu ya fedha.
 
Pia kuna baadhi ya watu wakipata mishara utajua tu kwa kuona matumizi yao wanayoyafanya. Kufanya hivo ni Kujirudisha nyuma mwenyewe jambo lamsingi la kufanya juu ya matumizi sahihi ni kuwa na mapagalio mzuri wa pesa nunua kitu ambacho umepanga kununua. Pia Hakikisha ya kwamba kila pesa unayoipata na kuitumia Unaiandika katika daftari lako la kumbumbuka hii itakusaidia kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha maana utakuwa unajua kila faida na hasara ya jambo unalolifanya.
 
Kukopa pesa ovyo
Hili ndilo kosa kubwa ambao linawaelemea watu wengi sana. Nadhani utakuwa shaidi mzuri ni jinsi gani! madeni yanavowatesa au yanavokutesa. Wapo baadhi ya watu wanakopa pesa katika taasisi za kifedha lakini hawana elimu ya kutosha juu ya mikopo hiyo hasa katika kuangalia mkopo utakuwa na faida au hasara. Wengi Hawaelewi kuhusiana na mkopo hasa swala zima la kulipa riba.
 
Utashangaa kwa mfano mtu anakopa shilingi laki tisa na anatakiwa kurudisha milioni moja ndani ya mwezi mmoja. Kwa kuwa pesa hiyo haukujua juu ya riba hiyo pindi unaposhindwa kuirejesha utajikutana unanguna na wale wanaosema pesa ni shetani.
 
Maana yangu ni kwamba kukopa sio kubaya ila jaribu kupata elimu ya kutosha juu ya mikopo na jaribu kufanya uchunguzi wa mkopo hasa swala la riba. Jaribu kufanya mlinganisho kutoka taasisi moja na nyingine hii itakusaidia kujua ni mkopo gani unakufaa.
 
Tukiachana maswala ya mikopo katika mataasisi ya kifedha wapo baadhi ya watu ni wakopaji wazuri kwa watu wengine kama vile nguo, viatu na pesa. Usiwe na madeni ambayo yamezidi kwa kiwango kikubwa kwani kuwa na madeni kwa kiasi kikubwa yanakurudisha nyuma kwa namna moja au nyingine.
 
Back
Top Bottom