Facebook kwa kawaida imekuwa hairuhusu watoto wa chini ya miaka 13 kutumia mtandao wake mkuu wa Facebook.
Lakini taarifa zinasema wapo wengi ambao huhadaa kuhusu umri wao na kwamba inakadiriwa watoto zaidi ya 20 milioni wa chini ya miaka 13 wanatumia mtandao wa Facebook.
Messenger Kids inatarajiwa kuwapa watoto ufahamu kuhusu nembo ya Facebook na hivyo kuongeza uwezekano wao kusalia kwenye mtandao huo. Facebook wamechukua hatua hiyo huku wakiendelea kupata ushindani mkali kutoka kwa Snapchat.
Facebook wamesema utafiti unaonesha wazazi wako radhi kuwaruhusu watoto wao wa miaka 6 hadi 12 watumie mitandao ya kijamii, mradi wawe wanaweza kufuatilia watoto wao wanafanya nini.
Akaunti ya mtoto inaweza kusimamia na mzazi kwa kutumia akaunti yake ya Facebook.
Watoto wataruhusiwa kuwasiliana kwa video, kutuma picha, video na arafa kwa marafiki zao ambao wameidhinishwa na wazazi wao.
Kujianika inaweza kuwa na definition tofauti kwako na kwake Mkuu. Kumbuka tamaduni za nchi na nchi zinatofautiana sana lakini kutokana na technology tofauti za tamaduni zinazidi kupungua siku hadi siku. Zamani ningekwambia huyu atakuwa si muafrika lakini wako Waafrika kibao ndani ya Afrika ambao "wanajianika" mitandaoni. Dunia ya leo imevaa tambara bovu.
Leukemia ni Saratani ya damu ambayo huanzia kwenye mafuta au urojo wa mifupa na kusababisha uzalishaji wa chembe hai za damu zisizo kawaida kwa wingi na kusababisha upungufu wa damu, kuvuja damu na mwili kushindwa kupigana na maambukizi mbali mbali.
Saratani hii hauambukizwi bali hurithiwa kutokana na mabadiliko katika DNA ambayo huathiriwa na mionzi mikali, maambukizi ya virusi, kemikali hatari na matumizi ya tumbaku na sigara kwa muda mrefu.