Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

IMG-20171206-WA0045.jpg
 
ambacho husababishwa na minyoo iitwayo Schistosoma mansoni ambao hupatikana katika mishipa ya damu ya utumbo”
“Dalili kuu za Kichocho cha mkojo ni kuwepo kwa damu katika mkojo, kujisikia hali ya mwili kuchoka, kuwa na kikohozi kikavu na maumivu ya misuli
 
pia dalili za Kichocho cha tumbo ni kuharisha kinyesi chenye damu, maumivu ya tumbo na kuvimba tumbo” anaeleza Dkt. Nzalawahe.
Kama nilivyoeleza awali Kichocho huwapata binadamu pamoja na wanyama wafugwao kama Ng’ombe, Mbuzi na Kondoo kiitwacho (Bovine Schistosomiasis) ambacho husababishwa na minyoo iitwayo Schistosoma
 
bovis waishio katika mishipa ya damu ya utumbo wa wanyama na kupelekea mnyama kupunguza hamu ya kula, kuharisha damu, upungufu wa damu, mnyama kukonda na asipopata tiba mnyama hufa.
 
JINSI YA KUJIKINGA NA UGONJWA WA KICHOCHO.

Ugonjwa wa kichocho unaweza kuzuiwa kwa urahisi iwapo kanuni za kiafya zitazingatiwa. Hata hivyo hadi sasa hakuna chanjo iliyopatikana ya kudhibiti ugonjwa huo. Si maji yote ni salama kwenye maeneo yaliyo na ugonjwa huu. Sehemu hatari zaidi za ugonjwa huo ni maeneo kama vile kingo za maziwa,
 
mito na mabwawa ambapo maji yametuama na kuna uoto wa mimea. Sehemu salama ni kama vile katika fukwe za bahari na zile zenye mawimbi ambazo si rahisi kukuta konokono wa majini. Mabwawa ya kuogelea ni salama iwapo yatanyunyiziwa dawa ya klorini.
 
Kuacha kujisaidia haja kubwa au ndogo kwenye mabwawa, mito, maziwa na mifereji ya maji. Kwa mtu mwenye kichocho (cha mkojo (Bilhazia) anapokojoa mkojo hutoka na mayai ya kichocho, na kwa kichocho cha tumbo,
 
haja kubwa huwa na mayai ya kichocho ambayo huanguliwa mara tu yanapogusana na maji na vijidudu vilivyo anguliwa huingia mwilini mwa konokono na kuendelea kukua, baada ya wiki tano hutoka na kurudi kwenye maji, ambako huogelea kutafuta mtu aliyepo ndani ya maji na huingia kwenye mwili wa mtu kupitia kwenye ngozi.
 
Kuacha kuoga, kuchota, kufua nguo kwenye maji yaliyotuama kama vile katika mabwawa, mito, maziwa na mifereji ambayo mingi inakuwa na konoko wanaosambaza kichocho. Badala yake watu wawekewe maji ya bomba ambayo huwekewa dawa za kuua vimelea vya maradhi.
 
Kuondoa majani yaliyoota kwenye maji sehemu ambazo watu huenda kuchota maji, kufua, na kuoga katika mabwawa, mito, maziwa, mifereji lengo likiwa ni kuharibu makazi ya konono.
 
Back
Top Bottom