Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

KICHOCHO NI NINI?

Kichocho ni ugonjwa unaosababishwa na minyoo midogo aina ya Schistosoma au Bilhazia. Minyoo ambayo huingia katika mwili wa binadamu kwa njia ya vitundu vya ngozi na kusababisha mwasho katika viungo mbalimbali vya mwili. Hivyo kupelekea homa, mwili kudhoofu,
 
kupungukiwa kinga mwilini na hatimaye mtu kupoteza maisha.
Pamoja na binadamu kuonekana kuugua ugonjwa wa kichocho pia wanyama wafugwao kama vile Ng’ombe, Mbuzi na Kondoo hupatwa pia na ugonjwa huu wa kichocho wanapotumia maji yaliyo na vijidudu vya maradhi hayo.
 
KICHOCHO KINAENEZWAJE?

Minyoo aina ya Schistosoma ambayo hueneza Kichocho cha mkojo hasa kwa binadamu inatokea katika Konokono waishio katika maji. Kichocho cha mkojo kwa binadamu husambazwa na konokono wajulikanao kama Bulinus africanus,
 
Bulinus tropicus na Bulinus forskalli, konokono hawa pia husambaza kichocho cha ng’ombe. Kichocho cha matumbo cha binadamu husambazwa na konokono waitwao Biomphalaria pfeiferi.
“Schistosoma lava wakiwa katika maji hutoboa ngozi ya binadamu au mnyama aliyeingia katika maji hayo na kuingia hadi kwenye mishipa ya damu mpaka kufika kwenye maini ambapo hapo hubadilika
 
na kuwa minyoo ambayo itaendelea kukua na kuelekea katika sehemu mahsusi ya mwili ambapo minyoo wakubwa hukaa ” anasema Dkt. Jahashi Nzalawahe kutoka idara ya Vetenari Microbaiolojia na Parasaitolojia ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA.
 
IMG-20171206-WA0048.jpg
 
AINA ZA KICHOCHO

“Kuna aina kuu mbili za kichocho ambazo ni kichocho cha mkojo na kichocho cha tumbo, Kichocho cha mkojo (Urinary schistosomiasis) husababishwa na minyoo inayoitwa Schistosoma haematobium ambao huishi katika mishipa ya damu ya kibofu cha mkojo cha binadamu na Kichocho cha matumbo (Intestinal schistosomiasis)
 
Back
Top Bottom