Kwa wakulima wanaofanya kilimo cha umwagiliaji yafaa wavae mabuti na gloves kujikinga na vijidudu vya kichocho kujipenyeza kwenye ngozi. Njia nyingine ni kunyunyizia dawa za kuua konokono kwenye maji (ziwa, mto, bwawa, mfereji), wenye konokono waenezao kichocho.
Ni vyema tujue kuwa, mtu anapaswa kumuona daktari baada ya kuwa na dalili za ugonjwa na yeye ndiye atakayemuainishia dawa za kutumia. Ni matarajio yetu kuwa iwapo tutafuata kanuni na misingi yote hiyo ya kiafya hapo juu, basi tutafanikiwa kushinda vita dhidi ya maradhi ya kichocho. Kwa kufanya hivyo maambuki ya kichocho yanawezwa kuzuiliwa na hatimaye ugonjwa huu kuweza kuteketezwa kabisa