Ugonjwa wa uti wa mgongo hutokea iwapo utando unaofunika ubongo na uti wa mgongo utapatwa na maambukizi.
Ugonjwa wa Uti wa mgongo husababishwa na nini?
Ugonjwa huu husababishwa na vimelea mbalimbali vya makundi ya bakteria, virus na hata fungus. Tukivigawanya visababishi hivi katika makundi haya, tutaona kuwa bakteria wanaosababisha ugonjwa wa uti wa mgongo ni kama vile; bakteria wajulikanao kama Beta-streptococci,
Hemophilus influenza, Escherichia coli, Listeria monocytogenes, Neisseria meningitides, Streptococci pneumoniae pamoja na Mycobacteria tuberculosis, ambao pia ni maarufu kwa kusababisha ugonjwa wa kifua kikuu.
Aidha kutoka kundi la virus, virus wanaojulikana kwa kusababisha ugonjwa huu wa uti wa mgongo ni pamoja na Herpes simplex type 2, HIV pamoja na Varicella zoster.
Vimelea vya fungus ambavyo hujulikana kwa kusababisha ugonjwa wa uti wa mgongo ni pamoja na wale wajulikanao kama Coccoidiodomycosis pamoja na Cryptococci meningetides.
Mgonjwa kupatwa na degedege (seizures) na mwili kukakamaa
Mgonjwa kushindwa kuvumilia mwanga (photophobia)
Mgonjwa kutoweza kukaa sehemu yenye makelele (phonophobia)
Kwa watoto, kuvimba utosi
Mgonjwa kupatwa na degedege (seizures) na mwili kukakamaa
Mgonjwa kushindwa kuvumilia mwanga (photophobia)
Mgonjwa kutoweza kukaa sehemu yenye makelele (phonophobia)
Kwa watoto, kuvimba utosi
Aidha, wakati wa kumfanyia mgonjwa uchunguzi, daktari anaweza kuangalia pia viashiria vingine vinavyoonesha kuwepo kwa ugonjwa wa uti wa mgongo. Ishara hizi ni kama vile
Mgonjwa uhisi maumivu kwenye uti wa mgongo yanayozuia kukunjua goti wakati anapofanyiwa uchunguzi wa kukunjua goti lake (pain limits passive extension of the knee). Ishara hii huitwa ishara ya Kerning au Kerning's sign.
Wakati mwingine mgonjwa anapoelekezwa kujitahidi kukunja shingo, miguu (yaani paja pamoja na goti) navyo hujikunja pia (flexion of the neck causes involuntary flexion of the knee and hip). Ishara hii huitwa ishara ya Brudzinski au Brudzinski’s sign.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.