Kadhalika matatizo unayokutana nayo ni kengele inayokutaka kujifunza kitu katika safari yako ya maisha, na hivyo chukua hatua kwa kujifunza suala husika.
Mfano, ukiandamwa na madeni mengi, chukulia kuandamwa huko na madeni kama kengele inayokutaka ukae chini na ujifunze kuhusu fedha. Kwa mtizamo huu furaha itadumu ndani yako na utajenga imani kubwa ya kufanikiwa.
Maana chochote kitakachokuvuruga utakipuuza mara tu baada ya kufikiria mafanikio ya ndoto yako unayoyatekeleza. Ukiweza kuunganisha imani ya kufika ndoto yako na hisia zako ni wazi utakuwa na furaha kila mara.
Tano; Thamani mahusiano yako na wengine.
Jali sana mahusiano yako ya ndoa, ndugu zako, marafiki zako, wafanyakazi wenzako, jamaa zako na jamii kwa ujumla.
Usimpuuze mtu yeyote wathamini wote, hii itakuchochoa kuwa furaha kila mara. Wote hao watakusamini na kukupenda hivyo furaha itakuja kama tunda la thamini unayowapa.
Sita; Jenga afya yako ya kiroho.
Ili ni eneo muhimu sana katika hali ya kuwa na furaha na kufanikiwa. Ukiwa vizuri kiroho utakuwa vizuri pia kihisia kwa sababu hakuna furaha ya ajabu kama kuwa karibu na Muumba yaani Mungu Mwenyezi, yeye ambaye ni asili ya uwepo wetu. Kila roho ina kiu na Mungu.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.