Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hatimaye, kola inayoning’inia ikaanza kutumiwa badala ya kitambaa cha shingoni. Hii ilikuwa kola nyeupe iliyofunika bega zima na ilining’inia juu ya mkono. Kola hizo ziliitwa pia Vandykes. Miongoni mwa wengine, zilivaliwa na Wapiuriti.
 
Kitambaa hiki kilizungushwa kwenye shingo zaidi ya mara moja. Ncha zake zilining’inia mbele ya shati. Michoro ya mwishoni mwa karne ya 17 huonyesha kwamba skafu zilipendwa sana wakati huo.
 
Skafu zilishonwa kwa kitambaa cha pamba, bafta, na hata gidamu. Zile zilizoshonwa kwa gidamu zilikuwa ghali. Yasemekana James wa Pili wa Uingereza alilipa pauni 36 na shilingi 10 kwa ajili ya skafu moja siku ya kutawazwa kwake, bei ghali mno nyakati hizo.
 
Mtindo huu wa tai uliitwa solitaire. Fundo hilo lilishabihi bow tie ya kisasa. Yasemekana kwamba kulikuwa na angalau njia mia moja za kufunga skafu. Yasemekana kwamba Mwingereza Beau Brummell, aliyechangia sana mitindo ya mavazi ya wanaume, alitumia asubuhi nzima kufunga skafu moja ili kuhakikisha iko sawa kabisa.
 
Kufikia miaka ya 1860, skafu yenye ncha ndefu ilianza kushabihi tai za mtindo wa kisasa na ikaitwa tai. Pia iliitwa tai yenye fundo la kitanzi. Jina hilo lilitokana na fundo lililotumiwa na madereva wa gari lililokokotwa na farasi wanne. Shati zenye kola zikawa ndio mtindo.
 
Watu fulani waweza kuwa na maoni hususa kuelekea mtu wasiyemjua ikitegemea aina ya tai anayovalia. Hivyo, ni jambo la hekima kuvalia tai safi zenye vigezo au rangi zinazofaana na shati, suruali, au jaketi lako.
 
Ni nadhifu na la kiasi nalo hukubaliwa katika sehemu nyingi kunapokuwa na sherehe rasmi. Fundo jingine linalopendwa ni fundo pana isivyo kawaida, ambalo ni kubwa kwa kadiri fulani. Kwa kawaida kibonyeo kidogo hufanyizwa kwenye tai chini tu ya fundo.
 
Wanaume wengi hawapendi kufunga tai. Hawapendi kusongwa kwenye shingo zao. Hata hivyo, wengi ambao wamepatwa na tatizo hilo wamegundua kwamba saizi ya shati ndiyo humkosesha mtu starehe. Ikiwa una tatizo hilo, hakikisha kwamba kola ya shati yako si ndogo sana. Inapokuwa ya saizi inayofaa, huenda hata usitambue kwamba umefunga tai.
 
Katika nchi nyingi tai huonwa kuwa sehemu muhimu ya mavazi rasmi au ya kazi. Kwa sababu hiyo wanaume wengi Wakristo huvalia tai wanapojihusisha na sehemu mbalimbali zilizo rasmi za huduma yao. Naam, tai yaweza kumwongezea mwanamume adhama na kumfanya aheshimike.
 
Ukiwa umeshikilia sehemu ya mbele ya fundo bila kuikaza kwa kidole cha shahada, vuta upande mpana ndani ya pindo kuelekea mbele.
 
Back
Top Bottom