Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

NADIR HAROUB AULA YANGA


Naodha wa klabu ya Yanga, Cannavaro yuko mbioni kusaini mkataba mpya wa miaka miwili, kupitia mtandao wa Salehe Jembe umeripoti kuwa mazungumzo kati ya mchezaji na klabu yamefikia hatua nzuri na muda wowote Cannavaro atamwaga wino
 
MATHEO ANTHONY AOMBA KUONDOKA YANGA


Mshambuliaji wa Yanga raia wa Zanzibar, Matheo Anthony amekutana na kocha wake mkuu Lwandamina na kumuomba ruksa ya kuondoka katika dirisha dogo la usajili, klabu kadhaa kama Lipuli zimeonesha nia ya kuitaka huduma ya nyota huyo
 
SIMBA NA AZAM ZAANZA KUZUNGUMZA NA MWASHIUYA



Klabu za Simba na Azam zimeingia katika vita ya kumtaka winga wa Yanga, Mwashiuya ambaye amebakiza miezi sita mkataba wake umalizike na mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara, winga huyo amethibitisha wakati akifanya mahojiano na gazeti la Champion
 
SIMBA YALETA BEKI KUCHUKUA NAFASI YA MAVUGO


Klabu ya Simba ipo kwenye hatua za mwisho kumalizana na beki kisiki raia wa Ghana, Malik Ismaila wa Tema Youth, kwa mujibu wa Mwanaspoti umeripoti kuwa nyota huyo tayari yupo Dar es salaam na dili lake likifanikiwa anatarajiwa kuchukua nafasi ya Laudit Mavugo ambaye anatarajiwa kutolewa kwa mkopo katika klabu ya Gor Mahia
 
STAND UNITED YAANZA KUIJIIMARISHA

Kupitia gazeti la michezo la Mwanaspoti limethibitisha kuwa klabu ya Stand United ya mkoani Shinyanga imemalizana na mshambuliaji wa Vital'O ya Burundi, Ndikumana Selemani
 
NYOTA WA SERENGETI BOYS ASAIN MTIBWA

Nyota wa Serengeti Boys, Nickson Kibabage amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuendelea kuichezea klabu ya Mtibwa, kwa mujibu wa mtandao wa binzubeiry
 
JONAS SAKUWAHA MBIONI KUMALIZANA NA SIMBA



klabu ya Simba ipo kwenye harakati za kumalizana na mshambuliaji wa Zesco, raia wa Zambia Sakuwaha, nyota huyu tayari yupo Tanzania kwa ajili ya majaribio yanayotarajiwa kuanza siku ya Ijumaa ya Disemba 2
 
ASANTE KWESI KUSAINI YANGA KWA MILIONI 33


Mlinzi wa Lipuli yupo tayari kujiunga na klabu ya Simba endapo klabu hiyo italipa milioni 33
 
USENGIMANA AITAMANI YANGA



Straika wa Singida United Danny Usengimana, amewashangaza viongozi wa timu hiyo, baada ya kusema anatamani siku moja kuwa mchezaji wa Yanga
Usengimana ameiambia Goal, Haruna Niyonzima, ndiyo aliyemfanya aipende timu hiyo inayotumia rangi za njano na kijani, pamoja na mafanikio iliyokuwa nayo timu hiyo.
 
YANGA YAVUTIWA NA MZAMBIA




Klabu ya Yanga imevutiwa na huduma ya mshambuliaji wa Nkana Rangers ya Zambia, Adam Ziriku raia wa Ghana, straika huyo pia ananyemelewa na klabu ya nchini Afrika Kusini, Baroka Fc anayochezea Mtanzania Abdi Banda, kwa mujibu wa gazeti la Mwanaspoti la Jumamosi Disemba 2
 
KIPA WA YANGA KUREJEA TIMU YAKE YA ZAMANI?



Kuna uwezekano mkubwa wa kipa namba mbili wa Yanga, Kakolanya kurejea Prisons baada ya kupoteza namba mbele ya Youthe Rostand, kupitia ukurasa wake wa Instagram, kipa huyo amekuwa akiweka picha zake za zamani mara kwa mara akiwa na Tanzania Prisons hivyo kureta ishara kuwa yuko mbioni kurejea
 
MILIONI 70 KUMPELEKA MZAMIRU YANGA?

Kwa mujibu wa Mwanaspoti limeripoti kwamba mabosi wa Yanga wapo nchini Kenya kwenye kambi ya Kilimanjaro Stars kwa ajili ya kumshawishi kiungo wa Simba, Mzamiru Yasin naokujiunga
 
NJOMBE MJI YAWATAKA NYOTA WAWILI WA YANGA

Baada ya kumnasa kinda wa Serengeti Boys kwa mkopo, Nickson Kibabage, Njombe Mjiimehamishai nguvu zake kwa nyota wengine wawili wa Yanga, Yusuph Muhilu na matheo Anthony
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…