Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Gazeti la Daily Monitor la nchini Uganda limeripoti kuwa familia ya Ivan iliajiri walinzi kulinda kaburi hilo kwa kuwalipa kiasi cha shilingi milioni 1 za Uganda kwa mwezi ambapo tangu afariki mwezi May walinzi hao wamelipwa kiasi cha shilingi laki 6 tu za Kiganda.
 
Sadick Japhari, mkazi wa Tabora amepandishwa kizimbani kwa tuhuma za kufanya mapenzi na binti yake mwenye umri wa miaka 16 hatimae kumsababishia ujauzito na kukatisha masomo yake akiwa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari ya Lwanzari Tabora mjini.
 
Mtuhumiwa huyo alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Tabora na kupandishwa kizimbani kwa mara nyingine tena shauri lake namba 49 la mwaka 2017 likiwa upande wa kutolea ushahidi kwa upande wa Jamhuri ambapo ilikuwa ni zamu ya kutoa ushahidi kwa Afisa mtendaji wa mtaa wa shule Kata ya Kaloleni,
 
Hata hivyo kwa kuwa Afisa Mtendaji wa mtaa ambaye alikuwa na jukumu la kufuatilia watoto wanaoacha masomo kwasababu mbalimbali akuchukua hatua ya kumrejesha Tabora binti huyo na hapo ndipo alipojiridhisha kuwa ni mjamzito na siku chache baadae akajifungua mtoto wa kiume.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…