jinenee mazuri.
Hili ni jambo ambalo wengi hawalifahamu lakini linanguvu sana. Kujinenea mema ni moja ya njia ya kuufanya ubongo kutoa nguvu kubwa ya ndani iliyojificha kukusaidia kutatua changamoto zilizo mbele yako.
Epuka kusikiliza habari asubuhi.
Unapoamka asubuhi ubongo uko tayari kupokea agenda itakayoongoza mwelekeo wa fikra na mawazo yako. Ukianza na habari hasa za kwenye redio na televisheni hatari yake ni kwamba habari nyingi katika midia zetu huwa ni habari hasi.
Habari nyingi utasikia sijua maafa sehemu fulani au migogoro kule nakadhalika. Hivyo kuanza siku na habari utaelekeza fikra na mawazo yako kwa siku nzima kuwa na mwelekeo hasi tu.
Epuka kabisa mabishano. Mara nyingi asubuhi hutumika na watu wengi kubadilishana mawazo hasa ya yale ambayo usiku wote watu waliyasikia au kuyaona kwenye televisheni.
Katika muda huu ndipo mijadala na mabishano huzuka. Sasa kama unataka kuilinda siku yako epuka kujihusisha na stori hizo ambazo hupelekea mabishano. Mabishano haya huwa ni ya michezo, siasa, au ujuaji wa mambo.
Amka mapema sana. Ili njia zote hizo hapo juu zifanikiwe ni lazima uanze kujenga mazoea ya kuamka asubuhi sana, amka alfajiri kabla ya wengine. Hii itakusaidia kufanya mambo yako kwa ufanisi zaidi kuliko kufukuzana na muda.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.