Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uelewa mdogo wa watu ndiyo unaowafanya kupata saratani kwa kutokuwa na uelewa wa kutosha juu ya visababishi na namna ya kujiepusha na visababishi hivyo, pia tiba endapo watabainika wamepata saratani. Kuna aina nyingi za saratani na siyo ugonjwa mmoja kama wengi wanavyofahamu.
 
Saratani inatokea baada ya seli za mwili zinajizalisha/kuongezeka kupita kiasi na mahali zinapojizalisha ndiyo hufahamika kama aina ya kansa, mfano saratani ya matiti au saratani ya maini.
 
Seli hizo za mwili zilizoongezeka kupita kiasi husababisha madhara na kuvifanya baadhi ya viungo vya mwili kushindwa kufanya kazi vizuri. Matokeo yake utasikia mgonjwa anashindwa shughuli zake kwa sababu hiyo
 
Ukungu. Hata katika maisha upo [emoji124]‍♂️[emoji124]‍♂️[emoji124]‍♂️
5d8a7867dfa632666a3c2c22067a2079.jpg
 
Saratani inasababishwa na mionzi mikali ya jua au mionzi mingine.

Mtu anapopigwa na mionzi ya jua au mionzi mingine kwa muda mrefu anakuwa kwenye hatari zaidi ya kupata saratani. Seli zinazosababisha saratani zinasafiri sehemu mbalimbali za mwili na kusababisha madhara kwenye viungo.
 
Ulaji mbaya nao ni hatarishi kwa saratani. Baadhi ya watu wanakula bila mpangilio na kunenepa kupita kiasi. Unene kupita kiasi ni moja ya mambo hatarishi ya saratani, mtu anaweza kuepuka hatari hiyo kwa kufanya mazoezi ya viungo.
 
Vilevile virusi mbalimbali ikiwamo vya Ukimwi vinaweza kumsababishia mtu aina fulani ya saratani. Chama cha Saratani cha Marekani (ACS) kinaeleza kwamba watu wenye virusi vya Ukimwi wako kwenye hatari zaidi kupata maambukizi ya saratani.
 
Sababu zote hizo nilizozitaja zinatokana na mitindo mibaya ya maisha ambayo watu wengi wanafanya bila kuchukua tahadhari. Angalau siku hizi watu wenye ualbino wanasisitizwa kutumia mafuta maalumu ili kujikinga na mionzi ya jua ambayo inawasababishia saratani ya ngozi kwa urahisi zaidi.
 
Back
Top Bottom