JPM alitoa msamaha kwa baadhi ya wafungwa alipokuwa akihutubia Taifa kusherehea miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania Bara na miongoni mwa waliopata ahueni hiyo ni Babu Seya na Papii Kocha.
Babu, babu, babu,” zilikuwa ni kelele za mashabiki na ndugu zake waliompokea Babu Seya na Papii Kocha waliokuwa wametoka gerezani wakiwa na magitaa yao mgongoni.
Babu Seya aliyeonekana mtanashati alionekana anapunga mkono wa kulia kama mtu asiyeamini huku Papii Kocha akipunga mkono akionekana kufurahia na kuzungumza na mashabiki.
Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es Salaam, Augustino Mboje amesema kuwa hivi sasa wanakamilisha taratibu za kumtoa gerezani Nguza Viking na mwanaye Papii Kocha.
Ndugu hao ambao wameonekana wakiwa kwenye magari huku wengine wakizunguka zunguka nje ya gereza hilo kusubiria taratibu za wanamuziki hao kukamilika ili waachiwe.
Ndugu hao ambao wameonekana wakiwa kwenye magari huku wengine wakizunguka zunguka nje ya gereza hilo kusubiria taratibu za wanamuziki hao kukamilika ili waachiwe.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.